Sunday, December 15, 2013

DSC09909Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
KLABU ya Kagera Sugar yenye makazi yake Kaitaba mjini Bukoba inatarajia kuingia kambini baada ya sikukuu ya krimasi kujiwinda na mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi Januari 25 mwakani.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange amesema waliamua hivyo ili kuondoa usumbufu kwa wachezaji kufikiria kurejea majumbani kwao wakati wa mapumziko ya sikukuu halafu kurudi kambini tena Kaitaba.
“Wachezaji wetu wanatoka maeneo tofauti ya Tanzania. Tuliona ni usumbufu kuwaita kambini halafu kuwapa tena mapumziko wakati wa sikukuu ya krismasi. Uongozi ulitazama na kutathimini kwa umakini na kuamua kuwaita baada ya sikukuu”. Alisema Kabange.
Kabange alipoulizwa kama muda huo utatosha kuandaa kikosi chao kufikia januari 25, alijibu kuwa watakuwa na mwezi mmoja zaidi kuelekea kuanza mzunguko wa pili na hakuna shida juu ya hilo.
“Tumepiga hesabu, usidhani tulikurupuka kufanya maamuzi. Mwezi mmoja unatosha kwetu kujiandaa, hatuna `presha`”. Alisisitiza Kabange.
Aidha kocha huyo alisema mzunguko wa pili wanatarajia kufanya vizuri kwani wachezaji wao watakuwa wameshazoeana vizuri tofauti na mzunguko wa kwanza ambao ulikuwa mgumu kwao kufuatia mabadiliko ya kikosi.
Wakati kocha huyo akitamba kufanya vizuri, naye mshambuliaji wa klabu hiyo, Them Felix alikaririwa na mtandao huu akitamba kuendelea kufumania nyavu  mzunguko wa pili.
Felix alikiri ukali wa washambuliaji waliopo juu yake katika ufungaji wa mabao, lakini alisisitiza kuwa toka ligi kusimama amekuwa akipiga `Tizi` mchangani.
Msimu uliopita ambao Yanga walitwaa ubingwa, Kagera Sugar waliishia nafasi ya nne nyuma ya Simba Sc, wakiwa chini ya kocha aliyeondoka baadaye, Abdallah Kibadeni, lakini msimu huu wameonekana kutokuwa na makali.
Kwa sasa wakata miwa hao wapo chini ya kocha Raia wa Uganda, Jackson Mayanja akisaidiwa na Murage Kabange.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video