Rasimu ya Katiba hii ni ndefu kuliko ya kwanza in ibara 271 ya kwanza ilikuwa na ibara 240 .Wananchi wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala bora kama ifuatavyo:
1-lugha ya kiswahili ni Lugha ya Taifa.
2-Madaraka ya Rais yamepunguzwa.
3-Wabunge wasiwe mawaziri
4-Kuwe na ukomo wa wabunge
5-Wananchi wawajibishe wabunge
6-Spika/naibu wasiwe wabunge wala viongozi wa juu wa vyama vya siasa.
7-Kuwepo na jeshi moja la Polisi na Usalama wa Taifa.
MUUNGANO
Muungano umependekezwa uwe wa serikali tatu kutokana na kero mbalimbali zilizoko pande zote mbili.
Baadhi ya kero hizo ni kama ifuatavyo:
Kero za wazanzibar
1-Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Tanzania na hivyo kutumia mwanya huo kujipatia misaada toka nje
2-Mambo ya muungano yamekuwa yakiongezeka
3-Kumuondoa rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais
Kero za Tanzania Bara.
1-Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamuhuri ya Muungano
2-Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wazanzibar huku Tanganyika wanaruhusiwa
0 comments:
Post a Comment