Tuesday, December 10, 2013

……………………………………………………………………………………..
-Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
-Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
-Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sayansi na Teknolojia (TASJA).
-Mwakilishi wa Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC)
-Washiriki wa Semina, Mabibi na Mabwana. 

Awali ya yote ninayo furaha kubwa kujumuika katika tukio hili kama mgeni rasmi wa kufungua mafunzo haya kwa waandishi wa habari juu ya masuala ya mazingira na viumbe hai.
Nakipongeza chama cha Tasja kwa kuandaa semina hii kwa ufadhili wa UNESCO kwa eneo hili lina umuhimu mkubwa na changamoto mbalimbali.
Nimetaarifiwa kwamba semina hii itawapa uelewa zaidi na ujuzi kwa waandishi wetu kuweza kuandika kwa umahiri taarifa za mambo yahusuyo mazingira na viumbe hai.
Hili ni jambo la kupokelewa kwa mikono miwili kwani waandishi wa habari ni wadau wakubwa sana katika kutimiza azma ya Serikali katika kuhakikisha inatatua changamoto za kimazingira.
Pamoja na njia nyingine za kutatua changamoto hizo, swala la elimu kupitia vyombo vya habari ni muhimu sana, hivyo waandishi wakielewa vizuri masuala hayo basi watakuwa ni waelimishaji wazuri wa jamii na hivyo kufikia lengo kwa pamoja kama nchi.
Katika kipindi hiki Tanzania kama ilivyo kwa nchi zingine ambapo inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, juhudi kubwa zinahitajika kutoka kwa vyombo vyetu vya habari kuelimisha jamii juu ya kuzuia madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
Vyombo vya habari vinapaswa kutilia kipaumbele habari za mazingira kwa sababu swala hilo linaathari ya moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku na uchumi kwa ujumla.
Kwa mfano, majanga ambayo yameikumba nchi kwa miaka ya hivi karibuni kama vile mafuriko na ukame ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo kwa kiasi kikubwa yametokana na shughuli za kibinadamu.
Kampeni dhidi ya uharibifu wa mazingira na viumbe hai itafanikiwa sana endapo waandishi wa habari watazingatia huo umuhimu wa mazingira na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Hata hivyo, kwa waandishi wa habari kuweza kuandika kwa ushawishi mkumbwa juu ya masuala haya ni lazima kuwepo na mafunzo kama haya ili kuwajengea uwezo.
Imekuwa ni desturi kwa vyombo vyetu vingi vya habari kutothamini habari za mazingira na viumbe hai, jambo ambalo linaiweka nchi yetu katika hatari kubwa kwa sababu bila wananchi kuelimishwa, majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi yatazidi kuikumba nchi yetu na hivyo tutakuwa tukirudi nyumba kiuchumi.
Uchumi wetu utaathirika kutokana na majanga ambayo yamekuwa yakiharibu njia kuu za usafirishaji kama vile barabara na reli na mashamba ya mazao.
Serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa swala la utunzaji mazingira na viumbe hai linafuatwa.
Kwa mfano, kupitia sera yake ya utunzaji mazingira na pia miradi mbalimbali, Serikali imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi juu ya kuepuka kuharibu mazingira na viumbe hai.
Serikali inaahidi kuwa itaendelea kutoa ushirkiano mkubwa kwa vyombo vya habari na wadau wengine katika juhudi za kupambana na hali hii inayotishia ustawi wa mazingira na viumbe hai hapa nchini.
UNESCO, kama mdau binafsi, imekuwa mdau mkubwa katika harakati hizi hapa nchini kwani imeshirikiana na Serikali katika maeneo mbalimbali ya nchi katika utunzaji mazingira na viumbe hai.
Maendeleo ya uhifadhi wa mazingira yanaweza kuangaliwa katika taswira tatu. Moja ni ile inayotokana na juhudi za Serikali kutenga na kutunza maeneo ya kuhifadhi viumbe wanyama na mimea. Katika hili, Tanzania imefanya vizuri sana.  Kwa mfano, wakati Tanganyika (Bara) inapata uhuru kulikuwa na maeneo ya hifadhi za wanyama 11  hivi sasa Bara inayo 32; ambayo pamoja na hifadhi za misitu ni takribani asilimia 35% ya ardhi ya nchi nzima.
Taswira ya pili ni ile ya kushirikiana na nchi nyingine kuhifadhi mazingira ya dunia kwa ujumla. Kwa hili pia Tanzania inaonekana kufanya vizuri katika uhudhuriaji wa makongamono na kuridhia mikataba na itifaki mbali mbali za kimataifa. Nyingi za rasmu hizi zimetaifishwa kuwa na hima ya sheria nchini, japo utekelezaji wake unakuwa mgumu kutokana na utegemezi wa rasilimali na teknolojia. 
Taswira ya tatu ni ya uhifadhi wa mazingira yanayomgusa binadamu moja kwa moja; hususan makazi, shughuli na maeneo yanayomzunguka na kugusa maisha yake. Hili ndilo eneo ambalo Tanzania haijafanya vizuri kiasi kwamba kuna athari za kimazingira zaidi leo kuliko ilivyokuwa kwenye miaka ya 60. 
Naomba nisiwachoshe kwa hotuba ndefu, baada ya kusema hayo natamka rasmi kwamba mafunzo haya sasa yamefunguliwa rasmi.
Asanteni sana kwa kunisikiliza, nawatakia kila la kheri katika kujifunza masuala haya ya utunzaji mazingira na viumbe hai.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video