





Na Nathan Mpangala
Help for Underserved Communities Inc. (HUC), imefadhili wanafunzi 11 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Morogoro kozi mbalimbali za ufundi zinazotolewa VETA, ambapo baadhi yao wameshaanza mafunzo na wengine wanatarajiwa kuanza Januari mwakani.
Akizungumzia ufadhili huo, Rais wa asasi hiyo, Bi. Zawadi Sakapalla – Ukondwa, alisema, “ufadhili umelenga vijana wenye nia ya kujiendeleza lakini wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo kutokana na uyatima na wazazi au walezi kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha”.
Majina, kozi na mikoa wanayotoka vijana hao ni; Joseph Mboya, Saidi Makope, Yasini Musa (ufundi magari, Dar es Salaam), Neema Bungara (umeme wa magari, Dar es salaam), Francis Mustafa (ufundi magari, Morogoro), Hassan Bakari, Fadhili Munda (udereva, Dar es Salaam), David Mwasyeba (udereva wa pikipiki, Mbeya), Jamila Mwenda (usekretari/kompyuta, Dar es Salaam), Monica Mhelela (saluni na utengenezaji nywele, Dar es Salaam) na Rose Mawawa (ufundi cherehani, Dar es Salaam).
HUC ni asasi isiyo ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayosaidia upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa, maktaba za kijamii na vifaa vya elimu kwa maeneo yenye upungufu wa huduma za kujamii. Habari zaidi: https://www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA/412893725452394
0 comments:
Post a Comment