Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail na Suppersport.com
Tel:0712461976 au 0764302956
Alvaro Negredo ameifungia Manchester City bao la ushindi usiku huu dhidi ya Liverpool na kuendeleza ubabe wao katika dimba la Etihad.
Liverpool ambao wamekuwa wapinzani wa Man City nafasi za juu katika msimamo wa ligi kuu nchini England msimu huu walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 24 kupitia kwa Philippe Coutinho akipokea pasi nzuri kutoka kwa Raheem Sterling.
Lakini wenyeji walijibu mapigo katika dakika ya 31 baada ya beki wa kati na nahodha wa Man City, Vincent Kompany kuunganisha mpira wa kona uliochongwa Mhispania David Sliva.
Sherehe ya ushindi kwa City ilikuja dakika ya 45 baada ya mshambuliaji hatari Alvaro Negredo kufunga bao la pili kufuatia kazi nzuri ya Jesus Navas.
Huwezi amini mpaka saa 12 kasorobo jioni ya leo, Liverpool walikuwa kileleni mwa EPL, hivi sasa ni saa nne usiku wameporomoka mpaka nafasi ya nne katika msimamo na Arsenal wakirudi kileleni kama kawaida.
Kali zaidi wiki ijayo, Liverpool wataingia kwenye kibarua kizito dhidi ya vijana wa Jose Mourinho, klabu ya Chelsea ya London.
Baada ya mechi za leo, timu tano za juu ni kama ifuatavyo;
Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Arsenal | 18 | 12 | 3 | 3 | 36 | 18 | 18 | 39 |
2 | Manchester City | 18 | 12 | 2 | 4 | 53 | 21 | 32 | 38 |
3 | Chelsea | 18 | 11 | 4 | 3 | 33 | 18 | 15 | 37 |
4 | Liverpool | 18 | 11 | 3 | 4 | 43 | 21 | 22 | 36 |
5 | Everton | 18 | 9 | 7 | 2 | 29 | 17 | 12 | 3 |

Kikosi cha Man City usiku huu: Hart 7, Zabaleta 6, Kompany 7, Lescott 7, Kolarov 5, Y Toure 6, Fernandinho 7, Navas 8, Silva 7 (Garcia, 86), Nasri 6 (Milner 71, 6), Negredo 8 (Dzeko 76).
Kikosi cha Liverpool: Mignolet 6, Johnson 6, Sakho 7, Skrtel 6, Cissokho 5; Lucas 6 (Aspas, 81), Sterling 7, Henderson 7, Allen 6, Coutinho 6 (Moses, 67), Suarez 7.










0 comments:
Post a Comment