Monday, December 16, 2013

mandela+pixMarehemu Mzee Madiba 
RAIS wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela alizikwa jana Jumapili kijijini kwake, Qunu kwa heshima zote za kitaifa, kimataifa na kimila.
Mandela aliyeitoa Afrika Kusini katika dhuluma ya ubaguzi wa rangi uliokuwa unafanywa na Makaburu wa nchi hiyo alifariki dunia Alhamisi ya Desemba 5 mwaka huu.
Kiongozi huyo maarufu duniani alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu akiwa na umri wa miaka 95.
Mandela ambaye alikuwa mtu muhimu duniani amefanyiwa heshima kubwa na dunia mzima ambayo yote iliiungana katika kipindi cha msiba wake.
Viongozi karibu wa Dunia nmzima walifika Afrika Kusini katika shughuli ya kumuombea na kumuaga kiongozi huyo shupavu ambaye mfano wake haujatokea Afrika.
Viongozi wa mataifa makubwa wakiongozwa na Rais Barack Obama wa Marekani na wale wa mataifa madogo walifika Afrika Kusini ili kuungana na wananchi wa nchi hiyo katika msiba huo mkubwa.
Ni dhahiri kwamba Dunia kwa ilichokifanya kwa Mzee Mandela imefanya kile ambacho alistahili kufanyiwa mtu shujaa wa mfano wake. Dunia imeshirikiana katika kumuaga marehemu Mandela ambaye kifo chake kimewaunganisha hata wale walio na uadui wa asili duniani.
Pamoja na kwamba lilikuwa ni tukio la msiba lakini ilifurahisha kuona Rais Obama anasalimiana na Rais wa Cuba, Raoul Castro ambao nchi zao zina uhasama wa kihistoria.
Pia lilikuwa tukio la kufurahisha kuona mtalaka wa Mandela, Winnie Mandela akipigana mabusu na mke wa marehemu, Graca Machel mbele ya halaiki ya watu kwenye Uwanja wa FNB.
Ni matumaini yetu kwamba muungano huu wa Dunia katika kumuaga na kumzika Mandela utakuwa chachu ya kuondoa uhasama duniani ambao ni moja ya vikwazo vya maendeleo.
Tunatarajia kwamba watu wote duniani watatumia kifo cha Mandela kama njia ya kuleta amani, utulivu na kupeana faraja katika matukio mbalimbali duniani.
Dunia inapaswa kufuata maisha yale yalivyokuwa ambayo yalijaa imani, huruma na unyenyekevu wa hali ya juu kwa kila binadamu.
Mzee Mandela ametuachia usia mkubwa na wa aina yake wa kusameheana. Aliwahimiza wananchi wote wa Afrika Kusini wasameheane na waridhiane na walijenge taifa lao.
Yeye mwenyewe alisamehe licha ya kufungwa jela miaka 27 na utawala wa Makaburu, Mandela alipotoka alitangaza kusamehe na kukemea kulipizana visasi akisema kwamba si njia njema ya kuondoa matatizo. Mandela alikuwa na nguvu kubwa mabali na kupendwa na watu wote dunaini kwa kuwa Rais wa Afrika Kusini alikuwa na mamlaka ya kulipiza kisasi kama angetaka na hakukuwa na mtu wa kumzuia. Lakini, Mandela alichana na hilo na kusamehe na kuwataka wananchi wa nchi yake wasiaca,eheane jambo ambalo lilisaidia sana kuijenga Afrika Kusini yenye nguvu dunaini.Wakati tunamaliza msiba wa Mzee Mandela ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuiga yote mazuri aliyoyafanya kwa faida yetu na kizazi kijacho cha Dunia.
Mtindo huo wa maisha ya kusameheana si muhimu kwa Afrika Kusini tu bali hata kwa Tanzania, Afrika na Dunia kwa jumla.
Iwapo watu wote duniani wataamua kumfuata Mandela kwa kusameheana Dunia itakuwa mahala pa kuzuri kwa kuishi na pepo ambayo inahadithiwa katika vitabu vya dini itaaanza kupatikana duniani.
Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu Mandela. Amina.
CHANZO: MWANANCHI

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video