Ama kweli makocha wajibu wao kufukuzwa!. Hatimaye kocha wa Watukutu wa Kaskazini mwa London, Tottenham Hotspurs, Andre Villas-Boas amefukuzwa kazi mchana huu bbaada ya kula kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 5-0 dhidi ya Liverpool dimba la White Hart Lane siku ya jana.
Taarifa inasema: ‘Klabu inatangaza kuwa makubaliano yamefikiwa na kocha mkuu Andre Villas-Boas, kusitisha huduma yake. Maamuzi yamefanyika kwa maelewano mazuri na kuzingatia faida kwa pande zote`.
“Tunamtakia kila la heri Andre katika maisha yake ya baadaye. Tutatoa taarifa zaidi baada kuhusu mrithi wake”.
Nje: Kocha wa Tottenham Hostpur, Andre Villas-Boas amefukuzwa kazi baada ya kulala mabao 5-0 dhidi ya Liverpool jana
0 comments:
Post a Comment