Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
WAUZA mitumba wa Ilala, klabu ya Ashanti United ya jijini Dar es salaam imetangaza vita ya kusaka nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara kufikia mwishoni mwa msimu huu wa 2013/2014.
Afisa habari wa klabu hiyo, Marijan Rajab amesema wameshaweka mikakati ya kuongeza nguvu zaidi chini ya kocha mpya, Alhaji Abdallah Kibadeni ` king Mputa` aliyetimuliwa na wekundu wa Msimbazi Simba SC.
Hapa ilikuwa siku ya kwanza kucheza ligi kuu msimu wa 2013/2014 ambapo Ashanti United walikula kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Yanga
“Ashanti tumejipanga vizuri sana, tumemchukua kocha bora kwa wakati wote, anajua soka la Tanzania, ana mbinu kubwa za kutufikisha mbali. Chini ya kocha Kibadeni, lazima tufanikiwe kupanda nafasi tano za juu”. Alisema Marijan.
Marijan alisema kuwa Ashanti walianza vibaya ligi kuu na kujikuta wakipasua vichwa kutafuta namna ya kurekebisha makosa kwa kubadilisha makocha bila mafanikio makubwa, lakini mzunguko wa pili wataanza kwa kasi.
“Tuko nafasi za mwishoni, lakini bado tuna mechi nyingine 13, zinatosha sana kutukusanyia mzigo wa pointi 26 na kukaa mazingira mazuri”. Aliongeza Marijan.
Ataifikisha Ashanti United nafasi ya tano?: Kocha Mpya wa Wauza mitumba wa Ilala, Alhaji Abdallah Kibadeni anatarajiwa kuifikisha timu hiyo nafasi ya tano
Afisah habari huyo alikiri wazi kuwa ligi ni ngumu sana kwani kila timu inajitahidi kufanya vizuri, lakini haiwapi shida kwa sababu walipanda ligi kuu kwa nia ya kushindana na si kushiriki tu.
Alipoulizwa hatari ya kushuka daraja, Marijan alitamba kwamba hiyo ni ndoto ya mchana, kamwe hawataweza kushuka daraja.
“Nakuambia ndugu yangu, kama kuna mtu anadhani tutashuka daraja, anaota mchana kweupe. Timu ina Kibadeni inashukaje daraja?. Sisi tuko fiti sana, vijana wameimarika sana na wanaweza kufanya kazi nzuri sana”. AlisemaMarijan.
0 comments:
Post a Comment