TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA
HABARI“PRESS RELEASE” TAREHE 07.12. 2013.
HABARI“PRESS RELEASE” TAREHE 07.12. 2013.
WILAYA YA KYELA - MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 06.12.2013 MAJIRA YA SAA 00:01HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUBAGA,
KATA YA BUJONDE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA MKOA WA
MBEYA. JAPHET S/O MWANGOLWA, MIAKA 83, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI
CHA LUBAGA ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI. MBINU NI KUMVIZIA MHANGA
AKIWA AMELALA NYUMBANI KWAKE NA MKE WAKE KISHA KUMUUA. CHANZO NI UGOMVI
WA UKOO KUGOMBEA MASHAMBA YA URITHI. WATUHUMIWA WATATU WALITAMBULIWA NA
MKE WA MAREHEMU WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI AMBAO NI 1. ALIPIPI
S/O MWANGOLWA, MIAKA 77, KYUSA, MKULIMA [AMBAYE NI MDOGO WAKE NA
MAREHEMU] 2. ANASTAZIA D/O NSOKA, MIAKA 40, KYUSA, MKULIMA [MKE WA
MTUHUMIWA] 3. EVARIST S/O ALIPIPI ULIMBOKA, MIAKA 30, KYUSA, FUNDI
UMEME [MTOTO WA WATUHUMIWA] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA LUBAGA – BUJONDE.
TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI
ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MATATIZO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA YA
MAZUNGUMZO NA KUJENGA HOJA BADALA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA PIA KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA
KATIKA JAMII.
[ BARAKAEL MASAKI - ACP ]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment