Kikosi
cha Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la
Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania
(Tanzanite) kinatua nchini kesho (Desemba 5 mwaka huu).
Afrika
Kusini itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South Africa Airways.
Wanaounda
Basetsana ni makipa Kaylin Swart, Regirl Ngobeni na Juliet Sethole.
Mabeki ni Abongile Dlani, Caryn van Reyneveld, Chamelle Wiltshire,
Meagan Newman, Nomonde Nomthseke, Tiisetso Makhubela na Vuyo Mkhabela.
Viungo
wapo Amanda November, Amogelang Motau, Gabriella Salgado, Koketso
Mamabolo, Nomvula Kgoale na Thembi Kgatlane. Washambuliaji ni Mosili
Makhoali, obyn Moodaly, Sduduzo Dlamini na Shiwe Nogwanya.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) ni sh.
1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C,
sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.
JOPO LA WATAALAMU KUPANGA MKAKATI WA AFCON 2015
Jopo
la wataalamu 20 walioteuliwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi linakutana kupanga mkakati wa kuonesha
jinsi Tanzania inavyoweza kushiriki Fainali za Afrika (AFCON)
zitakazofanyika mwaka 2015 nchini Morocco.
Kikao
hicho maalumu (retreat) kitafanyika mjini Zanzibar kuanzia Desemba 6-8
mwaka huu. Jopo hilo litaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Idd Omari Kipingu.
Wengine
wanaounda jopo hilo linalohusisha pia makocha ni Dk. Mshindo Msolla,
Peter Mhina, Ayoub Nyenzi, Abdallah Kibaden, Pelegrinius Rutahyuga,
Kidao Wilfred, Salum Madadi, Juma Mwambusi, Ken Mwaisabula, Boniface
Mkwasa, Fred Minziro, Meja Abdul Mingange, Ally Mayay, Boniface Mkwasa
na Dan Korosso.
Wajumbe wengine wa jopo hilo wanatoka Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA).
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment