Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
MABINGWA
watetezi na vinara wa ligi kuu vodacom Tanzania bara , Dar Young
Africans wanaanza kunoa makali yao novemba 25 mwaka huu ili kujiweka
sawa zaidi kuelekea mzunguko wa pili wa ligi hiyo pamoja na michuano ya
kimataifa.
Kaimu
katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesema klabu hiyo inakabiliwa
na michunao mikubwa na malengo yao ni kupata mafanikio zaidi ya miaka
ya nyuma, kuanzia ligi kuu na ligi ya mabingwa barani Afrika.
“Kwasasa
vijana wako likizo ya wiki mbili, watawasili novemba 24 mwaka huu,
program zote zitakamilika wakati huo ambapo benchi zima la ufundi
litakuweopo. Tuna mechi dhidi Ya Simba Sc katika kampeni ile ya Nani
Mtani Jembe, tunarudi kujiandaa vizuri, lakini pia tunajiandaa na
michuano ya ligi kuu na ligi ya mabingwa”. Alisema Mwalusako.
Mwalusako
aliongeza kuwa moja ya mikakati yao kwa sasa ni kusaka wachezaji wa
kuongeza kikosini, na kwa kuanza wamelamba dume, Kipa Juma Kaseja Juma
ambaye timu yake ya zamani, Simba sc ilishindwa kumwongezea mkataba mpya
baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita.
“Wewe
unamwonaje Kaseja?, kamati ya usajili ilipata mapendekezo kutoka benchi
la ufundi kuwa kipa huyu anafaa kutokana na kiwango chake na uzoefu
mkubwa, hivyo ataisaidia timu sana. Lakini pia tunapepesa macho huku na
kule kuangaliwa nyota wengine, wapo watu wa usajili wanafanya kazi yao
vizuri”
Kisichokufaa
wewe chamfaa mwenzio, Simba sc walisema kashuka kiwango na kupotezea
kumpa mkataba mpya, lakini watani zao Yanga wameona jamaa bado yumo
Kiongozi huyo amewaomba mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuipa sapoti timu yao kwani umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
Mwalusako
alisema ni jambo la kawaida kwa mashabiki kusikitika pale timu
inaposhindwa kufanya vibaya, na katika mazingira hayo misuguano
inakuwepo na mwisho wa siku kitu kimoja cha msingi kinapatikana.
“Mashabiki
wetu wana uchu wa mafanikio, tunatambua hilo, na ndio maana tunaongeza
nguvu zaidi. Cha msingi tuungane pamoja ili kufikia malengo yetu”.
Alisema Mwalusko.
Yanga
walimaliza mzunguko wa kwanza novemba saba mwaka huu kwa kuifunga mabao
3-0 klabu ya JKT Oljoro katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam na
kupanda kileleni mwa ligi kuu baada ya kufikisha pointi 28, tofauti ya
pointi moja na Azam fc wenye pointi 27 nafasi ya pili na Mbeya City
nafasi ya tatu wakijikusanyia pointi 27, tofauti ni wastani wa magoli ya
kufunga na kufungwa.
0 comments:
Post a Comment