Imeelezwa
kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wanaugua ugonjwa wa kisukari hali
ambayo huchangia na unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara, ulaji wa
vyakula usiofaa na kutokufanya mazoezi ya mwili.
Hayo
yamesemwa leo na Dk. Omary Ubuguyu kutoka Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili(MNH) wakati akitoa semina kwa waandishi wea habari kuhusu
ugonjwa huo leo jijini Dares Salaam.
Aliongeza kuwa asilimia ya idadi ya watu 80 hadi 90 wanaugua ugonjwa huo duniani.
“
Unywaji wa pombe kuanzia chupa tano kwa wanaume na chupa 4 kwa wanawake
huchangia kusababisha ugonjwa huu,” alisema Dk. Ubuguyu.
Kwa
upande wake Mratibu wa semina hiyo ,kutoka Mradi wa Taifa wa Kisukari,
John Gardner alisema gharama ya matibabu ya ugonjwa huo ugharimu dola
za Marekani milioni 378 ya asilimia 12 ya bajeti ya afya duniani kwa
mujibu wa takwimu za mwaka 2010, ambapo inaweza kufikia hadi zaidi dola
milioni 400.
Akizungumzia
kuhusu ugonjwa huo, Dk. Zakharia Ngoma alisema ulaji usiofaa na
mtindo wa maisha huchangia kwa kiasi kikubwa . Hivyo hutumiaji wa vya
kula vya asili , vya kuchemsha, mafuta, chumvi na sukari kidogo , mboga
za majani kwa wingi na matunda kila siku , pamoja na vyakula vyenye
virutubisho vyote husaidia kuepukana na ugonjwa huu,” alisema Dk. Ngoma.
Aliongeza
kuwa hutumiaji wa vyakula vya jamii ya kunde na visivyokobolewa
husaidia kuepuka ugonjwa huu, ikiwemo kunywa maji kwa wingi na kuepuka
msongo wa mawazo.
0 comments:
Post a Comment