Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Viongozi wa CCM
pamoja na wananchi wa wilaya ya Tunduru mara baada ya kuwasili kwenye
wilaya hiyoikiwa sehemu ya ziara yake ndefu katika mikoa ya kusini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia mikono na wananchi wa kijiji cha Nakapanya,wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Wananchi wakazi wa kijiji cha Nakapanya wakionyesha Korosho kama sehemu
ya kilio cha cha muda mrefu ambacho kimekuwa hakisikilizwi
ipasavyo,wananchi hao walimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana kwa uamuzi wake wa kulisemea na kuahidi kulishughulikia kwa Chama
kuibana Serikali juu ya masuala muhimu ya zao la krosho kwa kutasaidia
sana kuinua uchumi wa mikoa ya kusini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za wanachama
wa Chama cha CUF ambao wameamua kurudi rasmi CCM wakiongozwa na
aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,Sheikh Ally Hashim.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji
cha Nakapanya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambapo aliwaambia
wananchi hao kuwa Chama Cha Mapinduzi ilishatoa tamko la kuitaka
serikali ishughulikie matatizo ya zao la korosho mara moja na kusisitiza
kuwa Chama Cha Mapinduzi ni chama cha Wakulima na Wafanyakazi hivyo ni
jukumu la chama kuwatetea wakulima wa Korosho walipwe kwa wakati na kwa
bei nzuri,pia Korosho zibanguliwe nchini kwani zitaongeza thamani yake
na pia kupanua wigo wa ajira.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Nakapanya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
0 comments:
Post a Comment