Baada
ya karibia miezi sita kupita tangu Wajerumani wafurike Wembley kushudia
mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, wajerumani
wameonekana kutovutiwa sana na mechi ya kirafiki baina ya timu yao dhidi
ya England uwanjani hapo.
Msahabiki
wa Bayern Munich na Borussia Dortmund walivamia maelfu ya tiketi mwezi
mei mwaka huu, lakini mpaka sasa tiketi chini ya elfu moja zimeuzwa kwa
mashabiki wanaotarajia kusafiri kuishangilia timu ya kwenye mchezo wa
kirafiki wiki ijayo baina ya wapinzani wao wa siku nyingi, timu ya Taifa
ya England dimba la Wembley.
Mechi hiyo kali ya kirafiki ni maalumu kwa Chama cha soka nchini England, FA kuadhimisha miaka 150 .
Uwanja
ulitapika: Mashabiki wa Ujerumani walijaza uwanja wa Wembley mwezi mei
mwa huu kushuhudia Bayern Munich ikimtwanga Dortmund na kunyakua ubingwa
wa UEFA
Walijaa: Mshabiki walijaza uwanja wa Wembley wakati Bayern Munich wakitwaa ndoo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya
Mechi
ya jumanne haitarajiwi kuwa na upinzani mkubwa sana uwanjani, lakini
England bado ina matarajio ya watu zaidi ya elfu 80 watashuhudia mchezo
huo.
0 comments:
Post a Comment