Mratibu
wa programu ya Wafanye Watabasamu ambaye pia ni mchora vibonzo wa ITV,
Nathan Mpangala (mwenye pensi nyanya), akiingia katika Kituo cha Ukuzaji
Sanaa cha Koko’TEN kilicho Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga, Jumamosi
iliyopita. Mpangala, alifuatana na wachoraji wenzake Abdul King O wa
gazeti la Nipashe na Said Michael wa Tanzania Daima kuendesha mafunzo ya
uchoraji kwa watoto wilayani humo. Kwa matukio zaidi bofya; https://www.facebook.com/nathan.mpangala

Mchora
vibonzo na mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala akishea neno
na wachoraji wa baadae katika Kituo cha Ukuzaji Sanaa cha Koko’TEN
Wilaya ya Lushoto, Tanga Jumamosi iliyopita.

Mchora
katuni wa gazeti la Tanzania Daima, Said Michael almaarufu ‘Wakudata’
(kulia) nae hakubaki nyuma kushea ujuzi wake kwa watoto wa Lushoto.

Mchora
katuni wa gazeti la Nipashe, Abdul King O aka Kaboka Mchizi (kulia)
akimwaga mambo kwa wachoraji katuni wa kesho katika Kituo cha Ukuzaji
Sanaa cha Koko’TEN, Lushoto, Tanga, Jumamosi iliyopita.

Baada
ya kuwatabasamisha watoto wa Koko’TEN Art Centre, Wafanye Watabasamu
ikapata nafasi ya kushangaa maajabu ya Milima ya Usambara. Pichani,
mchora katuni wa gazeti la Nipashe, Abdul king O, akipata msaada wa
kingo ya barabarani ili kulingana kimo na mchoraji vibonzo wa ITV,
Nathan Mpangala.
Mkurugenzi
wa Koko’TEN Art Centre, Gadi Ramadhani (katikati) katika picha ya
pamoja na Wachoraji katuni Nathan Mpangala (mwenye kaputula rangi ya
Mnyama) na Abdul King O. Picha hii walipiga katika kilele cha Irente
View, juu ya Milima ya Usambara. Ukifika mahala hapa, barabara ya
Dar-Arusha inaonekana kama izi.


Milima ya Usambara ina mapango yanayotaka moyo kukatiza. (Picha zote hisani ya Wafanye Watabasamu)
0 comments:
Post a Comment