Katibu
Mkuu wa ITU ambalo ni Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia
Mawasiliano Duniani Dr. Hamadoun Toure akisikiliza Maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma. Kulia ni Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni
Waziri wa ICT wa Thailand.

Timu
ya Tanzania ikifanya mikakati ya kushiriki kikamilifu katika siku mbili
zilizobaki. Hapa wakipeana taarifa ya Matukio ya siku ya pili.
Na Innocent Mungy – Bangkok Thailand
Tanzania inashiriki katika
Kongano la TEHAMA la Dunia linaloandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa
linalosimamia Mawasiliano Duniani (ITU-International Telecommunications
Union) linalofanyika katika jiji la Bangkok nchini Thailand.
Kongano hilo lenye Kauli Mbiu ya
Kuchochea Mabadiliko Katika Ulimwengu wa TEHAMA, unashirikisha nchi
wananchama wa ITU na wasio wanachama, Makampuni ya Mawasiliano Duniani,
Taasisi na wasimamizi wa sekta ya Mawasiliano Pamoja na Serekali,
wanashiriki Kongano hili katika kipindi ambacho mabadiliko makubwa
katika Sekta ya Mawasiliano.
Mabadiliko haya yanapelekea dunia
kuwa na Changamoto ya Kuyakubali Mabadiliko hayo na kukabiliana na
Changamoto zake kwani faida za mabadiliko ni kubwa kwa Jamii Habari
duniani. Akizungumza jijini Bangkok, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na
Teknolojia Prof. Makame Mbarawa amesema Tanzania iko tayari kwa na
imeshapokea mabadiliko na imetekeleza mikakati ya kuhakikisha Tanzania
inapokuwa mabadiliko bila tatizo.
Aidha Mheshimiwa Mbarawa amesema
Tanzania inatambua umuhimu wa mabadiliko katika TEHAMA hususan kipindi
hiki cha dijitali kwani ndio njia pekee ya kuharakisha maendeleo ya
watanzania kwa ufanisi.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma amesema Tanzania tayari mstari
wa mbele kuhakikisha inachochea mabadiliko ya teknolojia ya habari na
mawasiliano ili wananchi wafaidike na huduma za Mawasiliano. “Tuna mfumo
mzuri wa usimamizi wa leseni za muingiliano wa teknolojia, sheria na
kanuni nzuri ambazo zinawezesha mabadiliko katika TEHAMA kunufaisha
watanzania. Tayari Tanzania imeingia katika mfumo wa Utangazaji wa
digitali na tunaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuwepo kwa huduma
nyingi zaidi kurahisisha maisha ya watanzania”. Amesema Profesa Nkoma.
Taasisi kadhaa toka Tanzania
zinashiriki Kongano hili kutoka Tanzania ikiwa ni pamoja na W ziara ya
Afya, Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia, DTBi ya wavumbuzi na
wagunduzi, NICTBB inayosimamia mkongo wa Taifa, MaxCom.
Kongano hili linafanyika kwa siku
nne kuanzia tarehe 19 – 22 Novemba 2013. Tanzania inashiriki na kauli
Mbiu ya nchi “Tanzania: Africa Strategic ICT Hub”. Pamoja an Kongano pia
yako Maonesho ya ICT yenye nia ya kuonesha jinsi nchi zinavyochochea
maendeleo kwa raia wake kupitia TEHAMA. Banda la Maonesho la Tanzania
limevutia watu wengi wanafikia kujifunza jinsi Tanzania imeweza
kuchochea mabadiliko katika TEHAMA na jinsi wananchi wanafaidika na
huduma mbalimbali zinazotolewa nchini.
Aidha Baadhi ya Taasisi
zinazoshiriki zinaangalia uwezekano wa kuchochea zaidi upatikanaji wa
huduma zao kwa kuwa na washirika katika shughuli zao. Leo asubuhi Ujumbe
wa Tanzania ulishiriki katika Mkutano Maalum wa Wawekezaji Katika Sekta
ya Mawasiliano ulioendeshwa na Naibu Katibu Mkuu wa ITU Bwana Houlin
Zhao.
0 comments:
Post a Comment