Na Gladness Mushi, Arusha
MAMLAKA ya mapato mkoa wa arusha (TRA) imefanikiwa kuongeza kiasi cha
mapato yake ambapo Jumla ya Bilioni 205 zimefanikiwa kukusanywa kwa
kipindi cha mwaka 2012,2013 jambo ambalo limefanya mamalaka hiyo
kuendelea kupanua wigo zaidi wa kuhudumia wananchi wa Jiji la Arusha.
Hayo yameelezwa jana na Meneja wa
mamlaka hiyoEvarist Kileva wakati akiongea kwenye uzinduzi wa wiki ya
mlipa kodi ambayo inaendelea jijini hapa
Kileva alisema kuwa mamlaka hiyo
hapo awali kwa kipindi cha mwaka 2011/2012 walifanikiwa kukusanya kiasi
cha Bilioni 176 kama mapato lakini kutokana na juhudi mbalimbali ambazo
wamezifanya zimeweza kuongeza kiwango cha mapato hayo
Pia alisema kuwa mbali na
kufanikiwa kukusanya bilioni 205 lakini pia wameweza kuweka malengo ya
ukusanyaji wa mapato ambapo kuanzia mwezi Julai hadi September 2013
wameweza kukusanya kiasi cha Bilioni 58.021 tofauti na mwaka jana ambapo
kwa miezi kama hiyo waliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 43 na kutokana
na hali hiyo wameweza kuweka ongezeko la Bilioni 14.312 sawa na
asilimia 33.
Aidha akitaja changamoto ambazo
zinaikabili mamlaka hiyo alisema kuwa ni pamoja na baadhi ya
wafanyabiashara tena wakubwa kushindwa kulipa kodi zao kama inavyo
staili jambo ambalo nalo linachangia sana kupoteza maana halisi ya
mamlaka hiyo lakini hata Serikali kwa ujumla
Hataivyo alitaja changamoto
nyingine kuwa ni pamoja na baadhi ya wadau bado hawajaweza kuelewasheria
za kodi zinazostaili hasa zile za msingi hivyo hali hiyo inachangia
sana ugumu katika zoezi la ukusanyaji wa kodi
Naye mgeni rasmi katika uzinduzi
huo ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alisema kuwa
suala la ulipaji wa kodi sio suala la hiari basi ni suala la lazima na
wala halina rangi wala itikadi za kichama hivyo wananchi hasa
wafanyabiashara wanapaswa kujua na kutambua kuwa kwa kushindwa kulipa
kodi kutachangia malengo ya TRA lakini pia hata ya serikali kuweza
kukwama.
0 comments:
Post a Comment