Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mkoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI),(kushoto ) na Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za
Mitaa wakifuatilia mkutano wa waaandishi wa habari leo jijini Dares
Salaam kuhusu ujio wa wageni hao, ambao watakuwepo nchini kuanzia
Novemba 23 hadi 26, mwaka huu.
Jumla
ya wageni 70 kutoka China wanatarajia kufanya ziara nchini Tanzania ili
kudumisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya Serikali za Mitaa.
Kauli
hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi Tawala za Mkoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI), Hawa Ghasia wakati akizungumza na waaandishi wa habari
leo jijini Dares Salaam kuhusu ujio wa wageni hao, ambao watakuwepo
nchini kuanzia Novemba 23 hadi 26, mwaka huu.
Waziri
Ghasia alisema ujumbe huo utakutana na Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu
Mizengo Pinda na baadhi ya mawaziriwa sekta mbalimbali wakiwemo wakuu
wa mikoa,, makatibu wakuu tawala wa mikoa, mameya wenyeviti wa
halimashauri za jiji, Manispaa, miji na baadhi ya wakuu wa wilaya,
wakurugenzi wa halimashauri hizo.
Aidha
ameongeza kuwa kutakuwepo na mkutano mkubwa utakaofanyika Novemba 25
,mwaka huu kwenye Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dares Salaam.
“Lengo
la ujio huo ni kuanzisha rasmi ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa
za Tanzania na China. Kupitia umoja huo ushirikiano kati ya Serikali za
Mitaa za Tanzania na China utakuwa wa kimkakati zaidi. Ili kufanikisha
ziara hii Serikali Kuu imewataka wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za
Mitaa na Taasisi zilizoko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI
kubaini fursa za uwekezaji na kuaanda mipango yao ya kuanzisha miradi ya
maendeleo ,”alisema Waziri Ghasia.
Alisema
Tanzania itanufaika katika katika maeneo ya Uchumi, miundombinu mfano
barabara ,Biashara, Elimu ya Jamii, Sayansi, Teknolojia,Utamaduni na
maeneo mengine.
Waziri
Ghasia aliongeza kwamba kupitia ushirikiano huo kutakuwepo na utoaji
tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri 100 wa shule za msingi na 100 kwa
shule za sekondari.Pia kutakuwepo na ziara zaidi za watumishi wa
halimashauri hizo.
( Picha na habari na Magreth Kinabo)
0 comments:
Post a Comment