Taifa
Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika keshokutwa
Jumanne (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze
na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya
(FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa
timu yake haitacheza tena mechi hiyo.
Kikosi
cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari
kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.
Waamuzi
wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa
Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.
Stars
chini ya Kocha Kim Poulsen ipo kambini tangu Novemba 12 mwaka huu
kujiwinda kwa mechi hiyo. Kim amejumuisha kwenye kikosi chake wachezaji
watano wanaocheza mpira wa miguu nje ya Tanzania.
…5,000/- NDIYO KIINGILIO CHA KUISHANGILIA STARS
Kiingilio
katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji Tanzania (Taifa
Stars) na Zimbabwe ni sh. 5,000 wakati tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu
(Novemba 18 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mbali
ya kiingilio hicho cha sh. 5,000 ambacho ni kwa viti vya bluu na
kijani, viingilio vingine ni sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B,
sh. 15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000.
Tiketi
zitauzwa katika magari maalumu katika vituo vya; Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni
Kariakoo, Dar Live Mbagala, OilCom Ubungo, BMM Salon iliyopo Sinza
Madukani, Uwanja wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama, na
kituo cha mafuta Buguruni.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment