“PRESS RELEASE” TAREHE 23. 11. 2013.
WILAYA YA MOMBA – TAARIFA YA KIFO.
MNAMO
TAREHE 22.11.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA
MAPOROMOKO – TUNDUMA , KATA YA TUNDUMA ,TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA
MOMBA MKOA WA MBEYA. VENANCE S/O MARCO, MIAKA 35, MKULIMA, MKINGA, MKAZI
WA MTAA WA MWAKA – TUNDUMA ALIFARIKI DUNIA AKIWA ANACHIMBA SHIMO LA
KISIMA LENYE UREFU WA FUTI 30 BAADA YA KUKOSA HEWA. MAREHEMU ALIKUWA
AKIFANYA KAZI HIYO NA MWENZAKE SHUNGU S/O JIMSON, MIAKA 35, MNYIHA,
MKULIMA, MKAZI WA MTAA WA MERERANI – TUNDUMA AMBAYE ALISTUKA BAADA YA
KUSIKIA MWENZAKE AKIKOROMA AKIWA NDANI YA SHIMO. SHIMO/KISIMA HICHO NI
MALI YA MANJANO S/O KHONDA, MIAKA 38, MSAFWA, BIASHARA, MKAZI WA MTAA
WA MAPOROMOKO – TUNDUMA AMBAYE NDIYE ALIYEWAPA KAZI YA KUCHIMBA
KISIMA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI KUBWA
PINDI WANAPOFANYA SHUGHULI ZINAZOHUSIANA NA UCHIMBAJI HUSUSAN MASHIMO
YENYE KINA KIREFU ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBOZI – TAARIFA YA KIFO.
MNAMO
TAREHE 21.11.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
SUMBALWELA, KATA YA IHANDA,TARAFA YA VWAWA WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA. MTOTO JEMES S/O MGODE, MIAKA 6, MNYIHA, MKAZI WA KIJIJI CHA
SUMBALWELA ALIKUFA MAJI KATIKA MTO IKOMELA WAKATI AKIVUA SAMAKI NA
WATOTO WENZAKE WATATU NDANI YA MTO HUO. KATIKA TUKIO HILO MTOTO ENOCK
S/O SIMON, MIAKA 6, MNYIHA, AMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI WILAYA YA
MBOZI HALI YAKE INAENDELEA VIZURI. PIA WATOTO VISENTI S/O ASHERY, MIAKA
6, MNDALI NA ALEX S/O ELIAS, MIAKA 5, MNDALI WALIPATIWA MATIBABU NA
KURUHUSIWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII
HASA WAZAZI/WALEZI KUWA NA UANGALIZI MAALUM NA WA KARIBU KWA WATOTO
WADOGO HASA WANAPOKUWA KATIKA MICHEZO YAO ILI KUEPUKANA NA MADHARA
YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBARALI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 22.11.2013 MAJIRA YA SAA 14:45HRS HUKO ENEO LA IBARA – RUJEWA
MJINI KATA YA RUJEWA,TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA
MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. KHALFAN S/O JUMA,
MIAKA 30, MKULIMA, MZARAMO NA 2. MICHAEL S/O KIMWAGA, MIAKA 28, MKULIMA,
MSANGU, WOTE WAKAZI WA RUJEWA WAKIWA NA BHANGI KETE MBILI SAWA NA UZITO
WA GRAM 10. WATUHUMIWA NI WAVUTAJI WA BHANGI, TARATIBU ZINAFANYWA ILI
WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment