“PRESS RELEASE” TAREHE 17.11. 2013.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA POWERTILLER KUMGONGA MTEMBEA
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 16.11.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MBUYUNI, KATA YA MAPOGOLO, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI
MKOA WA MBEYA, POWERTILLER LISILOKUWA NA NAMBA, LIKIENDESHWA NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO
NUSURA D/O EVENARY, MIAKA 7, MSANGU, MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA
S/MSINGI MBUYUNI MKAZI WA KIJIJI CHA MBUYUNI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA KWA
MATIBABU. CHANZO KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA VYOMBO VYA MOTO ILI
KUEPUKA AJALI NA MADHARA YA KIBINADAMU YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO
HILI AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO
TAREHE 16.11.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO KATIKA ENEO IGAWILO,
KATA YA IDUDA, TARAFA YA IYUNGA, BARABARA YA MBEYA/TUKUYU JIJI
NA MKOA WA MBEYA, GARI T.993 CWS/T.352 ASF AINA YA FAW LIKIENDESHWA
NA DEREVA YASIN S/O SAID, MIAKA 32, MNYAMWEZI, MKAZI WA DSM, LILIACHA
NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA MOJA LA YUSUPH S/O ? PIA KUSABABISHA MAJERUHI KWA 1.DEREVA WA GARI
HILO, 2. HUSSEIN S/O MUSSA, MIAKA 33, MSAFWA, MKAZI WA DSM NA 3.SELEMAN
S/O SALEH, MIAKA 21, MKAZI WA KYELA. CHANZO KINACHUNGUZWA. MAJERUHI
WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA PAMOJA NA MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment