“PRESS RELEASE” TAREHE 15. 11. 2013.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 14.11.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO MBALIZI KATA YA BONDE LA
USONGWE, TARAFA YA USONGWE BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI, MKOA WA MBEYA, GARI T.318 BHS/T.897 BMG AINA YA BENBEN
LIKIENDESHWA NA DEREVA NURDIN S/O YUSUPH, MIAKA 33, MNGONI, MKAZI WA
DSM, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ELIZA D/O LOFA, MIAKA 60, KYUSA,
MKULIMA, MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI TEULE YA IFISI.
DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MOMBA – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 14.11.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA
KILIMANJARO –TUNDUMA KATA NA TARAFA YA TUNDUMA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA
WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, GARI T.211 ACB AINA YA VOLVO
LIKIENDESHWA NA DEREVA GWELOMO S/O KALINGA, MIAKA 34, MHEHE, MKAZI WA
DSM LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE,
JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 30-35 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA
AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MSUKUMA MKOKOTENI KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 14.11.2013 MAJIRA YA SAA 19:30HRS HUKO IGURUSI KATA YA IGURUSI,
TARAFA YA ILONGO BARABARA YA MBEYA/NJOMBE WILAYA YA MBARALI, MKOA WA
MBEYA, GARI T.284 BNZ/T.638 BPF AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA
MBITA S/O SAID, MIAKA 35, MYAO, MKAZI WA MBEYA, LILIMGONGA MSUKUMA
MKOKOTENI KIBOSI S/O MWAIPUNGU, MIAKA 35, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA
IGURUSI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA
HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. CHANZO MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA
GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment