“PRESS RELEASE” TAREHE 13.11. 2013.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SARE ZA JESHI.
MNAMO
TAREHE 12.11.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA
CHUNYA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA
TRAIPHONE S/O MWANG’ONDA, MIAKA 24 ,KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA VWAWA
WILAYA YA MBOZI AKIWA NA SARE ZA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA [JWTZ]
AMBAZO NI SURUALI MOJA, KOFIA MBILI NA FILIMBI MOJA. MBINU NI KUTUMIA
SARE HIZO KATIKA MATUKIO YA KIHALIFU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA
KUMILIKI/KUTUMIA SARE ZA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA BILA UTARATIBU
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI NA ATAKAYEBAINIKA HATUA ZA KISHERIA
DHIDI YAKE ZITACHUKULIWA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU
YA MTU/WATU/KIKUNDI KINACHOMILIKI SARE ZA MAJESHI YA ULINZI NA
USALAMA IKIWA NI PAMOJA NA SILAHA KWA NIA YA KUFANYA UHALIFU AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 12.11.2013 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA STENDI
KUU, KATA YA MBALIZI ROAD,TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA,
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA ANYELWISYE S/O JOHN, MIAKA
22, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MTAA WA MAJENGO AKIWA NA BHANGI KETE MOJA
SAWA NA UZITO WA GRAM 5. MBINU NI KUFICHA BHANGI KWENYE MFUKO WA
SURUALI. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment