
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI
mahiri wa muziki wa Injili Solomon Mukubwa atashiriki Tamasha la
Krismasi lililopangwa kufanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa Dar
es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa tayari wamemalizana na Mukubwa, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.
“Pia
tumemalizana na mwimbaji wa hapa nchini anaitwa John Lissu ambaye ni
mmoja kati ya waimbaji mahiri na wenye mashabiki wengi.
“Dhamira
yetu ni kuwa na wasanii wote wanaokubalika na mashabiki,” alisema Msama
na kuongeza kuwa Desemba 26 mwaka huu tamasha hilo litafanyika Uwanja
wa Jamhuri Morogoro.
Mukubwa
ametamba na albamu mbalimbali ikiwemo Usikate Tamaa, ambayo ina nyimbo
kama Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Moyo Tukuza Bwana,
Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri na Usikatae Tamaa.
Pia Mukubwa amewahi kutoa albamu mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.
Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio.
Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio.
Wasanii
wengine ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hilo la nyimbo za
kusifu na kuabudu ni Watanzania, Rose Muhando, Upendo Nkone na Upendo
Kilahiro wakati wa nje ni Ephraim Sekeleti wa Zambia.
0 comments:
Post a Comment