Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Sc, Kepteini wa zamani wa JWTZ, Zacharia Hans Poppe
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU
wa Msimbazi Simba SC wamewataka mashabiki wao kuwa watulivu wakati huu
wa dirisha dogo la usajili kwani kamati iko makini kutafuta wachezaji
makini kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Mwenyekiti
wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, kepteini wa zamani wa jeshi la
wananchi Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe ameuambia mtandao huu kuwa
kwa sasa wanahangaikia nafasi ya mlinda mlango na nia yao ni kusajili
kipa mzawa kujiandaa na utarabu mpya utakaoanza kutumika mwakani.
“Kama
utaratibu mpya utaanza kutumika mwakani ambapo nafasi za wachezaji wa
kigeni ni tatu tu na kipa lazima awe Mtanzania., lazima tutafute kipa
mzawa ili kujiandaa na sheria hiyo mpya”. Alisema Poppe.
Poppe
alisema tayari wameshapokea taarifa kutoka kamati ya ufundi na leo hii
watapata maono yao baada ya hapo na wao kamati ya usajili wataingia
kazini.
“Dirisha
dogo tunahitaji wachezaji wawili au watatu ili kuongeza nguvu zaidi,
tumeona wachezaji wengi wa kusajili, lakini tutaangalia maeneo muhimu
zaidi kwa sasa ikiwemo nafasi ya mlinda mlango”. Aliongeza Poppe.
Kepteini
huyo wa zamani wa JWTZ aliwataka mashabiki wa Simba kuwa na imani kubwa
na viongozi wao kwani wanafanya kazi kwa weledi mkubwa kwa malengo ya
kuifikisha klabu mbali zaidi.
“Wapo
wachezaji wengi wa kuwasajii, lakini mashabiki na wanachama waelewe
kuwa tunafanya kazi kuzingatia majukumu tuliyojipangia, hivyo watuamini
sana”. Aliomba Poppe.
Mwishoni
mwa mzunguko wa kwanza, baadhi ya mashabiki wa Simba na viongozi
walitaka kumrejesha aliyekuwa mlinda mlango wao Juma Kaseja Juma kwa
madai kuwa kipa wao wa sasa, Mganda Abel Dhaira hana ubora wanaoutaka
wao.
Dhaira
amekuwa katika wakati mgumu kutokana na shinikizo la kutaka aondolewe,
lakini kwa upande wake amekuwa akisisitizamkuwa yeye ni kipa bora na
kama anafanya makosa ni ya kawaida sana katika soka.
Lakini
wamemkosa Kaseja aliyeitumia Simba kwa miaka 10 na mwishoni mwa msimu
uliopita alinyimwa mkatana mpya na kukosa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu
kwani hakuwa na timu, ila kwa sasa ni jembe halali la Yanga baada ya
kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la milioni 40 za Kitanzania.
Yanga
SC wamemsajili Kaseja kutokana na uzoefu wake wa michuano ya kimataifa
ikizingatiwa kuwa mwkaani wao ndio wawakilishi wa Tanzania katika
michuano mikubwa ya klabu bingwa barani Afrika .
0 comments:
Post a Comment