Mwenyekiti
wa Washirika wa Maendeleo Balozi wa Sweden , Lennarth Hjeimaker
(kulia)akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkutano wa
kupitia utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS) ulioshirikisha na
Washirika wa Maendeleo(DPS) na wadau mbalimbali kutoka serikalini
uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini
Dares Salaam (kulia) Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum .
Na Magreth Kinabo
Serikali
imesema kwamba itaendelea kuelekeza rasilimali katika masuala ya
elimu, afya, kilimo ikiwa ni hatua ya kuweza kupunguza umasikini kwa
haraka ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto zilizopo katika
sekta mbalimbali .
Kauli
hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkutano wa mwaka 2013
wa kupitia utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS) ulioshirikisha
na Washirika wa Maendeleo(DPs) na wadau mbalimbali kutoka serikalini
uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini
Dares Salaam.
“Changamoto
inayotukabili ni kuleta maendeleo kwa haraka. Uchumi wa nchi unakuwa
kwa asilimia 7 lakini umasikini umepungua kwa asilimia 2,”alisema Waziri
huyo.
Alisema
changamoto inayoikabili serikali ili kukabiliana na umasikini nchini ni
kuhakikisha inaelekeza rasilimali zake ili ziweze kuzalisha ajira .Pia
kuangalia idadi ya watu kulingana na uchumi wa nchi.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri huyo kufuatia Mwenyekiti wa Washirika
wa Maendeleo Balozi wa Sweden , Lennarth Hjeimaker kueleza kuwa
hatua za kupunguza umasikini na upatikanaji wa huduma za jamii bado
ni ndogo ,kiwango cha ufaulu kwa shule za sekondari na msingi kushuka
na uwiano wa walimu na wanafunzi bado mdogo, zaidi ya nusu ya watu
vijijini wahapati maji safi na salama na upatikanaji wa nishati
vijijini bado ni changamoto.
Wadau hao pia wameishauri Serikali kuendelea kupambana na tatizo la rushwa nchini.
Katika
kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2012/2013 wadau hao walichangia
Dola za Marekani milioni 560 na mwaka huu wa fedha waliahidi kutoa Dola
za Marekani milioni 561 hivyo hadi sasa Serikali imeshapokea Dola za
Marekani milioni 290.2.
|
0 comments:
Post a Comment