Salha
israel mrembo alieng’ara miaka ya 2011 katika mashindano ya urembo
nchini,akiongea na washiriki wa Tanzania Top Model 2013 namna ya
kujiamini wakiwa katika jukwaa na kujibu maswali endapo watakabiliana na
vyombo vya habari.
Washiriki wakiwa katika picha ya paoja na Salha israel.Mrembo
Salha Israel atembelea kambi ya washiriki wa sindano la Tanzania Top
model iliopo katika hoteli ya Jb Belmont iliyopo maeneo ya posta kwa
lengo la kuwapa mbinu mbalimbali za kufanya vizuri jukwaani kwani
shindano hilo lina upinzani mkali kwa washiriki wenyewe kwa wenyewe.
Salha
alitoa mbinu mbalimbali za kujiamini kwa mwanamitindo awapo jukwaani
pamoja na mbinu za kujibu maswali kiusahihi kwa wanahabari ambapo
imezoeleka kwa washiriki wengi hushindwa kujibu maswali kiusahihi kitu
ambacho hupunguza ari ya shindano.
Fainali za mashindano haya zitafanyika desemba 7,pia washiriki
watapigiwa kura na wananchi ambapo namba maalumu itaolewa hivi punde
kumpigia mshiriki umpendae ili kumuongezea alama amabazo zitamwezesha
mshiriki wako ashinde.
0 comments:
Post a Comment