Na Samia Mussa
MALKIA
wa muziki wa injili nchini Rose Muhando, amesema kuwa mashabiki wake
watarajie mabadiliko makubwa katika Tamasha la Kimataifa la Krismasi
linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
na Dira ya Mtanzania juzi mwimbaji huyo alisema anatarajia kufanya
makubwa katika Tamasha hilo tofauti na alivyozoeleka katika matamasha
yaliyowahi kufanyika.
“Siku
ya Krismasi ni siku ya kuzaliwa mtoto wa kiume ambaye ni Yesu, unajua
mara nyingi mzazi anapojifungua huwa ni furaha ya aina yake, nitaitumia
siku hiyo kumuimbia Mungu kwa sababu ni siku muhimu,” alisema Muhando.
Rose
alisema kuwa kwa sasa amebadilika kila kitu ikiwa pamoja na staili za
uchezaji sambamba na kuimba nyimbo mpya tatu alizozikalisha kurekodi
hivi karibuni.
“Mashabiki
watarajie kupata mambo mapya kutoka kwangu kwa sababu nina amani ya
Mungu, imeniwezesha kufikia hapa nilipo,” alisema Rose.
Msanii
huyo alisema kuwa anamshukuru Mungu na anafuraha kubwa kupata nafasi ya
kushiriki katika Tamasha la Krismasi na atatambulisha nyimbo tatu mpya
ambazo ni Kamata, Shikilia na Usiniache ewe bwana.
Msanii
huyo nguli wa muziki wa injili ambaye anakubalika Afrika Mashariki,
alisema katika Tamasha hilo ataimba live ambapo anatarajia kuimba nyimbo
mbalimbali zilizopo katika albamu zake ukiwamo wa Utamu wa Yesu, si
salama, Nibebe na Jipange Sawa sawa.
Alipotakiwa
kutoa ufafanuzi kama kuna msanii wa nje anamhofia alisema kuwa
anajiamini na kile anachokifanya na waumini watarajie kwa sababu hivyo
hakuna mwimbaji yoyote atakaye muogopa siku ya tamasha hilo la
kimataifa.
0 comments:
Post a Comment