Hao
ni baadhi ya Wanafunzi ambao hawapo katika mfumo rasimu wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa KATAVI Dkt Rajabu Lutengwe aliyefika kuwatembelea
wakiwa darasani huko kijiji cha Luchima kitongoji cha kata ya maji moto.
Watoto
hao wa wafugaji wa kabila la kisukuma, wazazi wao wameondolewa kutoka
maeneo yaliyokatazwa kuishi na sasa wamehamia maeneo ya kijijini,
lakini eneo hilo halina shule ya Msingi ingawa umri wao unaruhusu
elimu ya Msingi na wengi wao wana miaka kumi na mbili.
Kwa
sasa wanapata elimu kupitia mfumo usio rasmi , hawajaandikishwa, vyumba
vya madarasa hakuna,madawati shida na huduma nyinginezo hapo
wanasomea nje iwapo mvua ikinyesha hatima yao haijulikani juhudi za
makusudi zinahitajika kuokoa kizazi hicho. Shule hiyo isiyo rasmi iko
umbali wa kilometa takribani 40 kutoka makao makuu ya kata.
Picha na Kibada Wakibada, -Mlele- Katavi
Na Kibada Kibada -Mlele Katavi
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe amemaliza ziara yake Katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na kutoa maagizo kwa watendaji wa
Vijiji na Kata kuwataka wasimamie utekelezaji wa shughuli za maendeleo
ili kuwalete wananchi maendeleo ya haraka .
Amesema
kushindwa kusimamia maagizo ya viongozi yanayotolewa katika mkoa ni
utovu wa nidhamu, haina maana kuendelea kupokea mshahara wa serilaki
wakati huwatimizi wajibu waliokabidhiwa na serikali kuhakikisha
wanawaletea wananchi wa Mkoa wa Katavi Maendeleo.
Alisema
kuwa Moja ya mikakati ya mkoa na malengo iliyojiwekea na kuhimiza
watendaji wote wa Vijiji , Kata , Tarafa , Halmashauri na Wilaya ni
kuhakikisha wanatekeleza ufyatuaji wa Tofali milioni moja kwa kila
kijiji, watoto kupata chakula shuleni, kuondoa tatizo la madawati,
kufuta utoro mashuleni, kuongeza kiwango cha ufaulu kufika lengo la mkoa
la asimilia sitini na lengo la Taifa pia asilimia Sitini, kutosikia
kuwa watoto wameacha shule kutokana na mimba , utoro mashuleni, ujenzi
wa maabara,hosteli vyumba vya madarasa na Nyumba za walimu pamoja na
kulima kilimo chenye tija kinachomkomboa mwananchi, lakini hayo yote
hayatekelezwi .
Ziara
hiyo imemchukua Dkt Rutengwe takribani wiki mbili kwa kuanza kutembelea
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo katika Kata za Karema, Ikola, Kapalamsenga, Mwese., Zote zipo
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda .
Kata
nyingine alizotembelea ni Kata ya Sibwesa,Katuma, Kabungu, Mpanda,
Mpandandogo na Mishamo ambapo alifanikikiwa kukagua ujenzi wa miradi ya
kilimo ujenzi wa ghala katika kijiji cha Mwese, Msitu wa asili
uliohifadhiwa katika kijiji cha Mwese unaotumiwa na wananchi wa Mwese
kwa matumizi ya kuhifadhi mazingira.
0 comments:
Post a Comment