Na Mwandishi Wetu
WAKATI
maandalizi ya Tamasha la Krismas yakipamba moto, Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Kayanza Peter Pinda amesema wazo la
kuanzishwa kwa Tamasha la Krismas ni zuri lenye lengo la kuwakutanisha
Watanzania mahali pamoja kuabudu na kuliombea Taifa lao dhidi ya mabalaa
yanayoitesa dunia likiwemo suala la ugaidi, utekwaji wa viongozi na
kuteswa kwa Watanzania.
Waziri
Mkuu Pinda ambaye ni maarufu kama mtoto wa Mkulima anasema kwamba
Tamasha hilo ni zuri na litakata kiu ya mashabiki wa Muziki wa Injili
nchini tanzania kwa sababu linawakutanisha kwenye uwanja mmoja waumini
wa madhehebu mbalimbali.
Waziri
Mkuu anasema tamasha hilo ambalo wazo la Muandaaji maarufu wa Matamasha
ya Injili nchini, Alex Msama linapewa baraka zote kwa niaba ya
serikali kwa kuwa lengo lake kuu ni kuwafanya Watanzania kuwa na hofu ya
Mungu katika maisha yao yote wanayoishi hapa duniani.
“Mimi
kama mwakilishi wa Serikali, kwa niaba ya serikali yangu ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, natoa Baraka zote kwa Tamasha hili na ninaomba
lifanyike kwa amani na utulivu ili lengo la kuanzishwa kwake litimie,”
anasema Pinda.
Mbali
ya Waziri Mkuu , Pinda baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wameiunga mkono kauli ya Waziri Mkuu inayowataka
Watanzania kujitokeza kwa wingi katika Tamasha hilo la Krismas.
Lengo
la kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo maaskofu, wanasiasa na watu
maarufu ambao wanaweza kulizungumzia ipasavyo Tamasha hilo ambalo lina
nia ya dhati ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa njia ya muziki
kwa Jamii yote ya Watanzania.

Mwanjelwa
anasema lengo la Tamasha hilo ni mkusanyiko wa watu wa aina mbalimbali
ambao wanakusanyika kwa ajili ya kusahau yale yote mabaya ambayo yana
dhamira ya kupoteza taswira ya Tanzania ambayo ni kitovu cha amani.
Dhamira
hiyo inatokana na sababu kwamba Tamasha hilo ni la Kijamii zaidi na pia
ni takatifu kwani linashirikisha waimbaji na wadau mbalimbali wa
Kimataifa ambao wanakutana kwa lengo la kuondosha tofauti zenye
kuashiria uvunjifu wa amani.
Mwanjelwa
anasema ujio wa waimbaji mbalimbali kutoka nje ya Tanzania kunachangia
kukusanya wananchi kutoka nchi mbalimbali ambao hujitokeza kwa ajili ya
kupata neno la Mungu na kuburudika, mikusanyiko hii pia huondoa ubaguzi
wa nchi kwa nchi.
Mbunge
huyo anasema kutokana na mipangilio ya kuigwa inayofanywa na Msama,
Serikali inatakiwa kuchangia nguvu zake katika kufanikisha mikakati
inayofanywa na Msama kwani mikusanyiko ya Amani kama hii ni muhimu sana
kwa utengamano wa Taifa na bara letu la Afrika.
“Serikali
inatakiwa kumuongezea nguvu Msama kwa anayoyafanya, anawaunganisha watu
wa mataifa mengi kwa lengo la kumtukuza Mungu na kutoa michango yao
kuwasaidia wanaoishi katika mazingira hatarishi,” alisema Mwanjelwa.
Mbunge
wa Igalula (CCM), Athumani Mfutakamba anasema Tamasha hilo linaleta
mshikamano, upendo pia linaunganisha waumini wa imani tofauti katika
mikusanyiko ya kumwabudu Mungu.
“Kwa
sababu waumini mbalimbali watapata elimu na burudani,ambayo itazidisha
upendo amani na mshikamano miongoni mwao kama viumbe wa mwenyezi
Mungu, aliwataka waumini wa dini zote wajiandae kwa ajili ya Tamasha
hilo ambalo ni la aina yake.
Mfutakamba
alisema kwamba upendo huo na amani vitakavyotangazwa kwenye mikoa yote
litakapofanyika Tamasha hilo, waumini wajiandae vilivyo na Tamasha hilo
ikiwa ni pamoja na kupata maonyo ya Mwenyezi Mungu kupitia Injili.
Mfutakamba
anasema hatua ya kuandaliwa kwa Tamasha hilo kunatokana na sababu
kwamba dhamira ya dhati ya waasisi wa nchi hii waliweka sheria na haki
ya kuabudu, kukusanyika na kwenda kokote utakako pasi na kuvunja
sheria.
Naye
Mbunge wa Newala, Kapteni, Geroge Mkuchika amesema ni jambo la kheri
kwa waandaaji wa Tamasha hilo kulifanikisha kwa sababu linakusanya
waumini mbalimbali.

Mkurugenzi
wa Msama Promotions ambaye ni muandaaji wa Tamasha hilo, Alex Msama
anapongeza jitihada za Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambao wanatambua mchango wake katika kufikisha ujumbe kwa jamii
kupitia muziki wa injili na mapambio.
Msama
anasema Tamasha hilo linalotarajia kufanyika kwenye mikoa mitano,
Desemba 25 litafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku
inayofuata litahamia Morogoro, Dodoma, Tanga na Arusha.
“Wadau
wa Dar es Salaam na mikoani wakae mkao wa kula kwa sababu nimejiandaa
vilivyo kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa kishindo,
natarajia kushirikisha waimbaji wa nchi mbalimbali ambao wataimba
‘live’,” alisema Msama na kuongeza.
“Tamasha
la Krismas litazungumzia Amani zaidi baada ya matukio kadhaa ambayo
yanatishia maisha, hali ambayo haimfurahishi Mwenyezi Mungu,” alisema
Msama.
Msama
anasema Tamasha la Krismas litashirikisha waimbaji mbalimbali wa
Tanzania na kutoka nje ya Tanzania, mfumo wa waimbaji utakuwa ni wa
kuimba live tofauti na ilivyokuwa katika matamasha yaliyopita.
Aidha
Msama anawataja waimbaji waliothibitisha kushiriki katika Tamasha hilo
ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro (Tanzania),
Ephreim Sekereti (Zambia) na Solomon Mukubwa (Kenya).
Msama
anamalizia kwa kueleza kwamba, fedha zitakazopatikana kwenye Tamasha
hilo zitasaidia ujenzi wa kituo cha wenye uhitaji maalum kama Yatima,
wajane na wanaoishi katika mazingira hatarishi kinachotarajia kujengwa
Pungu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment