Kaimu
Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu Bi.Aldegunda Komba akitoa ufafanuzi
wa ushiriki wa Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika
kwa mwaka 2013. Maadhimisho hayo yatafanyika Novemba 20 jijini Dar es
salaam.
Na Aron Msigwa – MAELEZO, Dar es salaam.
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa itaendelea na jukumu la kukusanya na
kutoa takwimu Bora zinazokidhi mahitaji na viwango vinavyokubalika
kimataifa ili kuiwezesha serikali na wadau mbalimbali kufanya maamuzi
sahihi katika mipango ya maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa shughuli
za kitakwimu Bi.Aldegunda Komba wakati akitoa ufafanuzi wa ushiriki wa
Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka 2013.
Bi.
Aldegunda amesema maendeleo ya serikali yoyote ile duniani yanategemea
uwepo wa takwimu Bora ambazo hurahisisha utungaji wa sera sahihi na
upangaji wa mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata vipaumbele na
fursa zilizopo.
Ameongeza
kuwa takwimu bora huiwezesha serikali kufanya maamuzi sahihi na
kutathmini mwenendo na mafanikio ya mipango mbalimbali inayopangwa na
kukidhi mahitaji ya wadau mbalimbali kwa kuwapatia taarifa za Afya,
kilimo, watu na makazi, taarifa za mapato na matumizi ya kaya.
Amesema
Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazothamini mchango wa takwimu kwa
maendeleo ya taifa inaungana na mataifa mengine barani Afrika
kuadhimisha Siku ya Takwimu Afrika ambayo huadhimishwa tarehe 18
Novemba.
Ameeleza
kuwa hiyo nchini Tanzania itaadhimishwa tarehe 20 jijini Dar es salaam
chini ya kauli mbiu isemayo “Takwimu Bora kwa Maendeleo ya Afrika”
ikilenga kuifahamisha jamii juu ya umuhimu wa matumizi ya Takwimu bora
katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.
Kuhusu
ufanisi wa ukusanyaji wa takwimu Bora wa Tanzanzania ikilinganishwa nan
chi nyingine barani Afrika Bi. Aldegunda amefafanua Ofisi ya Taifa ya
Takwimu hutoa takwimu zake kwa kuzingatia sifa mbalimbali za upataji wa
takwimu bora zikiwemo za matumizi ya mbinu na viwango vinavyokubalika
kimataifa.
Pia
ameongeza kuwa takwimu zote zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu
huakisi hali halisi ya eneo husika pia takwimu hizo hutolewa kwa wakati
maalum.
0 comments:
Post a Comment