Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.PICHA|MAKTABA
Tanga.Waziri wa Uchukuzi, Dk
Harrison Mwakyembe ametangaza vita rasmi na wafanyabiashara wanaoingiza
bidhaa za magendo kupitia bandari bubu mkoani Tanga na maofisa wa vyombo
vya Serikali waliopo kwenye mtandao huo.
Dk Mwakyembe aliwataka watambue
kuwa, kiama chao kimefika kwa sababu tayari Serikali inayo majina ya
wafanyabiashara na baadhi ya maofisa wa polisi, Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA) wanaotumika kufanikisha
upitishaji magendo.
Dk Mwakyembe ambaye aliwasili
Tanga juzi na kufanya ziara ya ghafla kutembelea bandari bubu zilizoko
mkoani hapa, alitangaza vita hiyo alipozungumza na maofisa wa TRA,
polisi, TPA na wafanyabiashara.
Alisema baada ya Serikali
kudhibiti Bandari ya Dar es Salaam, wafanyabiashara magwiji wa
upitishaji bidhaa za magendo wamehamishia nguvu zao Tanga.
“Natangaza
rasmi vita dhidi ya walio katika mtandao huo, watambue hatuwezi
kuruhusu Bandari ya Tanga, bandari bubu na mpaka wa Horohoro kuwa gulio
la walanguzi, wapitishaji dawa za kulavya na wahamiaji haramu,” alisema.
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment