Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI
wa Tamasha la Krismasi, Alex Msama amewataka wafanyakazi wake wa
makampuni yake kutangaza uzalendo wa hali ya juu kwa sababu tamasha hilo
nia yake ni kutangaza amani na upendo.
Akizungumza
na wafanyakazi wake hivi karibuni, Msama alisema tamasha hilo litakuwa
na wageni wengi kutoka nchi mbalimbali sambamba na viongozi wa Tanzania.
Msama
aliyasema hayo katika maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajia
kufanyika Desemba 25 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na baadaye
mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha na Kilimanjaro.
“Kila
mmoja mfanyakazi awe askari kwa mwenzake ili kufanikisha maendeleo ya
Tamasha hilo ambalo litakuwa na dhamira ya kusaidia wanaoishi katika
mazingira hatarishi,” alisema Msama.
Aidha
Msama alisema umakini utaongezeka zaidi katika suala la tiketi ambazo
zitatoka nje ya Tanzania kwa sababu ya kukwepa wizi unaofanywa na baadhi
ya wasilolitakia mema tamasha hilo.
“Tunajipanga
kutengeneza tiketi kutoka nje ya nchi ambazo zimepiga hatua zaidi
kimaendeleo ili kukwepa wizi unaofanywa na wajanja wachache wasiolitakia
mema tamasha hilo lenye lengo la kusaidia wenye uhitaji maalum,”
alisema Msama.
0 comments:
Post a Comment