Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
Bechi
la ufundi la maafande wa jeshi la kujenga Taifa wa mkoani Pwani, Ruvu
Shooting Stars limesema linahitaji kusajili wachezaji kadhaa katika
dirisha dogo la usajili lililofungiliwa jana ili kuongeza nguvu
kuelekea mzunguko wa kwanza.
Kocha
mkuu wa klabu hiyo, Charles Biniface Mkwasa `Master` , amesema kuwa kwa
sasa ni mapema kusema anamsajili nani na nani, lakini kwa kwa sababu
muda upo, anajaribu kutafuta wachezaji kulingana na mapungufu yake.
“Kuna
haja ya kuongeza, lakini bado sijaona wachezaji. Unajua timu yetuu bado
tunaijenga na tuna udhaifu mwingi sana hasa sehemu ya mlinda mlango,
ulinzi na ushambuliaji”. Alisema Mkwasa.
Mkwasa
aliongeza kuwa walipata nafasi nyingi zaidi mzunguko wa kwanza lakini
walizipoteza, walifungwa magoli mengi zaidi, na hii inamaanisha
ushambuliaji ni butu, pia wanahitaji kutafuta kipa mwingine.
“Usajili
unahitaji umakini mkubwa, benchi la ufundi tunahaha kutafuta wachezaji
watakaotufaa zaidi ili kuwa na nguvu kubwa mzunguko wa kwanza, kikubwa
mashabiki wawe na subiri kwani timu bado inajengwa”. Alisema Mkwasa.
Mkwasa alikiri ugumu wa ligi kuu kwa sasa kwani timu zimejiandaa vizuri na zinacheza soka zuri zaidi.
“Timu
zina kasi kubwa, kila mtu anasaka pointi tatu muhimu, najua ugumu
uliopo mbeleni, ninahitaji kuongeza nguvu zaidi na kufuta udhaifu
nilionao katika kikosi changu ili kuweza kuendana na kasi ya wapinzani
mara mzunguko wa pili utakapoanza”. Alisema Mkwasa.
Ruvu shooting ilianza ligi vizuri, lakini haijamaliza vizuri mzunguko wa kwanza kutfuatia kupata matokeo mabaya.
0 comments:
Post a Comment