Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiteta jambo na Mama Marianne
Lwanetzki raia wa Ujerumani alipomtembelea nyumbani kwake jana kujionea
maisha ya mama huyo ambae kwa sasa anaishi Mkoani Rukwa katika nyumba
yake inayoitwa ‘Kinder House” na watoto yatima 12 ambao aliamua
kuwachukua kutoka katika mazingira magumu na kuishi nao kama watoto
wake huku akiwapatia huduma mbalimbali za chakula, malazi, elimu na
tiba. Watoto hao yatima wapo wanaume sita na wanawake ni sita.
Katika
historia yake fupi Mama huyo alifika Mkoani Rukwa kwa shughuli za
kitalii na ndipo alipomuona mtoto mmoja katika moja ya kituo cha kulelea
mayatima akiwa na hali mbaya ya kiafya huku akiwa mgojwa sana, Aliamua
kumchukua mtoto huyo na kuishi nae hadi akapona ndipo aliposhawishika na
kuamua kuhamia Tanzania na kuchukua watoto wengine yatima hadi kufikia
12 ambao kwasasa amesema wanatosha kulingana na uwezo alionao.
Aliongeza kuwa
katika kuwalea watoto hao anatumia uwezo wake yeye binafsi pamoja
na misaada mbalimbali kutoa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa nchini
kwake Ujerumani.
Mtoto
Kastory Mabruki ambaye ametajwa kuwa na sifa mbalimbali ikiwemo
Uongozaji wa kwaya kama inavyoonekana pichani na hata uongozaji wa
midahalo”debate” mbalimbali shuleni kwao zikiwemo za wanafunzi wa
madarasa ya juu zaidi ya lile analosoma na kuzimudu vizuri. Katika
watoto hao 12 kila mmoja anaonekana kuwa na kipaji cha aina yake ambapo
Mama yao Mlezi anajitahidi kuviendeleza na kuvipa nafasi.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea kumpongeza Mama
Marianne kwa juhudi alizozichukua ambapo ameguswa sana na mpango huo wa
mtu binafsi kulea watoto kama familia moja tofauti na sehemu nyingine
nyingi ambazo taasisi ndizo zinazojishughulisha na vituo vya kulelea
mayatima. Mkuu huyo wa Mkoa amewaasa watanzania wenye uwezo kuiga mfano huo kusaidia jamii kuondokana na kero za watoto wa mitaani.
Picha Ndani: Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati mbele waliokaa)
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mama Marianne Lwanetzki (wapili kushoto
mbele waliokaa) raia wa Ujerumani na watoto yatima 12 alioamua
kuwachukua na kuwalea kama watoto wake wakitokea katika mazingira magumu
na ambao anaishi nao katika nyumba yake anayoiita “Kinder House”
iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Mama huyo anawapatia
watoto hao mahitaji yao yote ikiwemo chakula, malazi na elimu. Kulia ni
Katibu wa Mhe. Manyanya Frank Mateni.
Picha Nje: Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (watatu kushoto) akiwa kwenye
picha ya pamoja na Mama Marianne Lwanetzki (watatu kulia) raia wa
Ujerumani na watoto yatima 12 alioamua kuwachukua na kuwalea kama watoto
wake wakitokea katika mazingira magumu na ambao anaishi nao katika
nyumba yake anayoiita “Kinder House” iliyopo katika Manispaa ya
Sumbawanga Mkoani Rukwa. Mama huyo anawapatia watoto hao mahitaji yao
yote ikiwemo chakula, malazi na elimu. Wapili kulia ni Hamza Temba –
Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
Nyumba
hii inajulikana kama “KINDER HOUSE” ambapo kwa mujibu wa Mama mwenye
nyumba hii Marianne Lwanetzki ambae ni raia wa Ujerumani alisema neno
“kinder” kijerumani lina maana ya watoto. Mama Marianne amesema nyumba
hiyo ambayo ni kubwa ikiwa na eneo la kutosha ameshaiandikia kisheria na
kwamba ni urithi kwa watoto hao 12 anaowalea hata kama hatokuwepo tena
duniani basi hapo ndipo nyumbani kwao.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa akiagana na familia ya Mama Marianne Lwanetzki yenye
watoto yatima 12 pamoja na wafanyakazi wake wanaomsaidia kwenye shughuli
za malezi.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment