Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akishangiliwa na watoto wadogo (chekechea)
wa shule ya awali ya Carlton iliyoko Colombo, nchini Sri lanka wakati
Mama Salma na wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Madola walipotembelea
shule hiyo tarehe 16.11.2013.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Sri lanka Madame Shiranthi
Rajapakse ambaya pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa Shule za Carlton
nchini humo wakati walipokutana kwenye moja ya shule hizo iliyoko
Colombo tarehe 16.11.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa kwa ngoma wakati alipokuwa
anaingia Gangaramaya temple inayotumiwa na watu wa madhehebu ya Budha
nchini Sri lanka tarehe 16.11.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje
wa India Mama Louise Khurshid, na Mama Charlotte Scott, Mke wa Makamu
wa Rais wa Zambia wakipata maelezo kuhusiana na Gangaramaya temple
kutoka kwa Naibu Mkuu wa Temple hilo Van Kirinda Assage tarehe
16.11.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Kiongozi wa Gangaramaya Temple Van Kirinda Assage.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Dunya Liyanage,
8, anayesoma darasa la 3 katika Shule ya Msingi ya Meusnes iliyoko
mjini Colombo wakati Mama Salma na wake wa Marais kutoka nchi za madola
walipotembelea maonesho ya Kendraya tarehe 16.11.2013.
Wake
wa Marais na wakuu wa nchi za Jumuia ya Madola wakimwangalia mama
mmoja wa Sri lanka aliyekuwa akitwanga kwenye kinu wakati
walipotembelea maonesho ya Kendraya huko Colombo tarehe 16.11.2013.
Mama
Salma Kikwete akiwa pamoja na wake wa Marais kutoka nchi za Jumuia ya
Madola wakiangalia jinsi mwanaume na mwamamke wakishirikiana kufinyanga
vyungu
PICHA NA JOHN LUKUWI
0 comments:
Post a Comment