Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
MWIMBAJI
anayechipukia kwenye muziki wa Injili , anayetamba na wimbo wa `Ni
kwaneema na Rehema` Edson Mwasabwite amekiri kuwa wimbo huo umebadilisha
maisha yake kuanzia kipato, kujulikana miongoni mwa watanzania wengi,
ingawa hajafikia malengo yake.
Mwasabwite amesema hayo alipotembelea nyumbani kwa mhariri mkuu wa mtandao wa FULLSHANGWE, Baraka Mpenja na
kuweka wazi kuwa mpaka sasa ameuza nakala za kutosha za wimbo wake
uliomtoa katika tasnia ya muziki wa injili `Ni kwa Neema na Rehema`.
“Kwasasa
hivi pesa niliyokuwa naitafuta kwa mwaka, ninaweza kuipata kwa siku
moja. Hakika ni kwa neema kwani sikutegemea kama nitafika hapa nilipo
ingawa najiona ndio kwanza naanza safari katika muziki wa injili”.
Alisema Mwasabwite.
Mwasabwite
ameongeza kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiria kama Mwenyezi
Mungu angemshushia neema kama ilivyo sasa, kwani ametoka katika hali ya
kushindwa kununua hata baiskeli na sasa anafikiria kupata usafiri wake
wa kumsaidia kufanya kazi ya Mungu.
“Wimbo
huu umenibadilisha maisha yangu, kwasasa mashabiki wengi wa muziki wa
Injili wananihitaji kila sehemu ili nikafanye huduma. Kiukweli hata
ratiba zangu zimebadilika, nimekuwa nikihitajika maeneo mengi sana
kufanya matamasha, nami sichoki kwani nipo shambani mwa bwana”. Alisema
Mwasabwite.
Katika
mazungumzo yake, Mwasabwite amekiri kuwa kila jambo lina wakati wake,
Mungu hutoa kwa wakati wake, ikifika wakati wako utapata na hutaamini
muujiza utakaokutoea.
Mwimbaji
huyo anayesikika kila kona ya Tanzania aliongeza kuwa kwasa anajiandaa
kufyatua albamu mpya itakayobeba jina `Baba amenihurima asilimia Mia`.
“Nimeamua
kuipa jina hili kwasababu mimi kama Mwasabwite sijafanya chochote
zaidi ya Mungu kunihurumia na kunifikisha hapa nilipo kwa asalimia zote.
Sikuwa na sababu, vigezo, na nilikuwa wa kushindwa na kuaibika, kufa,
lakini mungu amenihurumia”. Alifafanua Mwasabwite.
Albamu
hii inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa nyimbo za injili itakuwa na
nyimbo 10 zenye ujumbe mkali wa kumsifu na kumtukuza Mungu.
Hata
hivyo, Mwasabwite amelalamikia suala la watu wachache kuiba kazi za
wasanii kwani huwa wanavuna wasipopanda, hivyo lazima mamlaka
zinazohusika kulinda haki za wasanii sanjari na serikali.
Pia amewasihii mashabiki kuungana na wasanii kununua CD Halisi ili kujenga uchumi wa wasanii na nchi kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment