Dar es Salaam.
Muuguzi aliyejitoa damu kuokoa maisha ya mjamzito Sista Hyasinta Baruti
na mume aliyemsindikiza mkewe kila alipohudhuria kliniki wakati wa
ujauzito Elia Mwumbui ni miongoni mwa Watanzania waliopewa tuzo ya
kuboresha afya ya mama na mtoto.
Tuzo
hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Madaktari Wahitimu Vyuo Vikuu vya
Tanzania (THPI), pia ilitolewa kwa Dk Faraja Mpwapwacha wa Lindi kwa
rekodi ya mama au mtoto kutokufa kwa miaka miwili wakati akizalisha.
Wengine
waliopata tuzo hiyo ni marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamini
Mkapa pamoja na Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete.
Pia tuzo hiyo ilienda kwa Mwenyekiti wa IPP, Dk Reginald Mengi kutokana na mchango wake katika mapambano ya saratani ya matiti.
Akizungumza
katika hafla ya utoaji tuzo hizo, Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib
Bilal ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema, nchi isipokuwa na raia walio
radhi kusimamia uhai wa wenzao nchi hiyo ni sawa na jangwa hasa katika
suala la afya.
Pia
Dk Bilal amesema, ushirikiano wa wadau mbalimbali wa sekta ya afya
utapunguza vifo vya mama na mtoto sambamba na maboresho ya utoaji wa
huduma hiyo nchini.
“Kama
kila mmoja wetu asipokuwa makini kusimamia uhai wa wenzake nchi hiyo ni
sawa na jangwa, hivyo tunawaomba wanaohusika na sekta ya afya
watekeleze wajibu wao ipasavyo” alisema Dk Bilal
Naye Mkurugenzi wa THPI, Dk Telesphory Kyaruzi alisema vifo vya mama na mtoto vimepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Alisema
jitihada hizo zitaendelea kufanikiwa ikiwa madaktari wazawa watakuwa
wazalendo na kufanya kazi nchini ili kuokoa maisha ya Watanzania
wanaopoteza uhai kwa kukosa huduma.
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment