Na Gladness Mushi, Arusha
CHUO
cha uasibu Arusha(IAA)kimesema kuwa kimefanikiwa kukusanya kiasi cha
zaidi ya Bilioni Moja kwa mwaka tofauti na hapo awali ambapo walikuwa
wanakusanya kiasi cha Milioni 20 kwa mwaka jambo ambalo limesababishwa
na ongezeko kubwa la wanafunzi .
Hayo
yamebainishwa na mkuu wa chuo hicho ambaye ni Profesa Johanes Monyo
wakati akiongea kwenye maafali ya nne ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni
hapo mapema jana.
Profesa
Monyo,alisema kuwa ongezeko la fedha hizo ni kutokana na kuwepo kwa
wanafunzi wengi tofauti na miaka ya nyuma ambapo na hivyo ongezeko hilo
limesababisha mapato nayo kuweza kukua kwa haraka sana.
Alifafanua
kuwa kinachosababisha waweze kupata ongezeko kubwa la wanafunzi tena
kwa kila mwaka ni kwa kuwa chuo hicho kinakugusa nyanja mbalimbali za
elimu wanayoitoa lakini pia wanashirikiana na vyuo vilivyoendelea
duniani katika kuwasaidia wanafunzi.
Alisema
ushirikiano baina yao na vyuo ambavyo vimeemdelea duniani kumesababisha
ongezeko lakini hata uwezo wa kufanya kazi kwa baadhi ya wahitimu wa
chuo hicho na hivyo kusababisha hata nchi ya Tanzania kuweza kupata sifa
lukuki mahala pa kazi.
Kutokana
na ongezeko hilo la wanafunzi katika Chuo hicho cha uasibu Arusha
alidai kuwa bado kinakabiliwa na changamoto lukuki ambazo kama zingeweza
kutatuliwa kwa haraka basi watanzia walio wengi zaidi wangeweza
kunufaika na chuo hicho na hivyo kusababisha hata matokeo ya haraka.
Alitaja
changamoto hizo kuwa ni pamoja na uhaba wa majengo ya kutosha ambapo
majengo yaliopo kwa sasa bado hayawezi kuwatosheleza wanafunzi wote
ukilinganisha na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaohitaji kujiunga na
chuo hicho kwa ajili ya kuweza kupata elimu.
Pia
alimalizia kwa kutaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na ukosefu wa
wahadhiri wa kutosha kwani waliopo kwa sasa bado hawatoshelezi mahitaji
ya chuo hicho.
0 comments:
Post a Comment