Makamu
wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika, wakati wakiwasili
kwenye ukumbi wa Mkutano wa Tatu wa nchi za Kiarabu ‘Afro Arab’,
uliofanyika nchini Kuwait, leo Nov 19, 2013. Picha na OMR

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihudhuria mkutano mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, ‘Afro Arab’ uliofanyika leo Nov 19, 2013, nchini Kuwait. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
(wa sita mstari wa tatu nyuma) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi
wa nchi mbalimbali za Afrika wakati alipohudhuria katika Mkutano wa
mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, ‘Afro Arab’ uliofanyika leo Nov 19, 2013 nchini KUwait. Picha na OMR
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kuwait City, Novemba 19, 2013
Makamu
wa Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal
ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa mashirikiano baina ya nchi za
Afrika na zile za Kiarabu, mkutano wa siku mbili unaofanyika katika
nchini Kuwait. Mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi wa nchi zaidi ya 70
unalenga kuimarisha ushirikiano wa Afrika na nchi za Kiarabu na
unapitia makubaliano ya mkutano wa Sirte, Libya uliofanyika mwaka 2011.
Mkutano
huu unafanyika kukiwa na mabadiliko kadhaa ya kiasiasa, kiuchumi na
kimkakati baina ya nchi za kanda hizi mbili huku taswira ya kukua kwa
ushikiano huu zikionekana bayana kuwa muhimu zaidi sasa kuliko
ilivyokuwa huko nyuma. Hii inatokana na nchi za kanda hizi mbili,
kukabiliwa na changamoto nyingi zinazofanana na zinazohitaji majibu ya
pamoja baina ya nchi za kanda hizi mbili. Baadhi ya changamoto hizo ni
pamoja na; mtikisiko wa uchumi, hali ya ulinzi na usalama, majanga
yanayoikabili dunia, usalama wa chakula na ugaidi.
“Changamoto
hizi hatuwezi kuzikabili wenyewe kama Tanzania ama kama Afrika.
Tunahitaji wenzetu wa ukanda huu wa nchi za Kiarabu kushirikiana nasi.
Katika umoja wetu tutafanikiwa kirahisi kuliko kama tutazikabili
changamoto hizi tukiwa tumejitenga,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Tanzania
licha ya kuwa na wananchi wake katika nchi mbalimbali za dunia, tawimu
zinaonesha kuwa, idadi kubwa ya wananchi hao wapo katika nchi za Kiarabu
hali inayoashiria umuhimu wa kukuza mahusiano baina ya Tanzania pekee
dhidi ya ukanda wa nchi za Kiarabu. Katika siku za hivi karibuni kupitia
Diplomasia ya Uchumi, Tanzania imefungua njia kwa wawekezaji wa nchi za
Kuwait, Oman na UAE na sasa taswira ya mahusiano ya Tanzania na nchi
hizi ni ya kuvutia ambapo inatoa fursa za kunufaika kiuchumi kwa
Tanzania kutoka katika ukanda huu kuliko kwa wadau wa maendeleo wa kanda
zingine ambazo Tanzania imekuwa ikishirikiana nazo.
Akizungumza
wakati wa kutoa taarifa ya kikao hiki kwa Makamu wa Rais, Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia yupo katika msafara
wa Mheshimiwa Makamu wa Rais, Bernard Membe alisema, kazi kubwa ya
mahusiano baina ya Tanzania na nchi za ukanda huu imejengwa na Rais
Jakaya Kikwete na sasa milango imefunguliwa kwa Watanzania kuchangamkia
fursa za maendeleo hasa katika suala zima la masoko ya bidhaa za kilimo,
ufiugaji na utalii.
Katika
Hotuba yake kwenye mkutano huu, Mheshimiwa Makamu wa Rais licha ya
kutoa shukrani na salamu za Tanzania kwa Amiri wa Kuwait, Sheikh Sabah
Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah na wananchi wa Kuwait na kwa viongozi wote
wan chi za kanda hizi mbili, Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua kuwa
Tanzania inatambua mahusiano ya kitamaduni, kihistoria na kijiografia
yaliyopo baina ya kanda hizi mbili na kwamba zaidi ya theluthi mbili ya
watu wa ukanda wa nchi za Kiarabu wanaishi Afrika hali inayochagiza
umuhimu wa uhusiano wa kanda hizi. Pia Mheshimiwa Makamu wa Rais
alifafanua kuwa, Mkutanouliofanyika Libya mwaka 2011, haukuonesha
mafanikio ya wazi hasa katika miradi ya Maendeleo na akauomba mkutano
huu wa Kuwait, kuhakikisha kanda hizi zinaongeza spidi ya kufanikisha
malengo ya kimaendeleo, ili wananchi wa kanda hizi wazidi kunufaika
kutokana na mahusiano haya.
Katika
msafara huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia ameambatana na Waziri wa
Kilimo na Chakula, Enginia Christopher Chiza, Waziri wa Ardhi, Makazi,
Maji na Nishati wa SMZ, Ramadhan Shaaban, Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara, Gregory Teu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Servacius Likwelile
na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa. Pia katika
msafara huo wapo wabunge Hamad Rashid na Khalifa Khalifa.
Imetolewa na: Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
0 comments:
Post a Comment