30/ 11/ 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko ya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja na baadhi ya Wakuu wa Upelelezi
wa mikoa na wakuu wa Polisi wa Wilaya katika baadhi ya mikoa hapa
Nchini.
Katika
mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna
msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya
Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia usalama wa
Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa kikosi cha
kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Aidha,
baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa Polisi wa
Wilaya(OCD) waliobadilishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa
makosa ya jinai mkoa wa Tabora ACP Edward Bukombe amehamishiwa Makao
Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Geita
(RCO) ACP Francis Kibona amehamishiwa mkoa wa Njombe kuwa mkuu wa
Upelelezi mkoa na nafasi yake inachukuliwa na SSP Simon Pasua kutoka
Makao makuu ya Upelelezi Dar es salaam.
Wengine
ni aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Wanging’ombe SSP.
Francis Maro amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa
na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Katavi ACP. Emmanuel Nley
amehamishiwa kikosi cha Polisi wanamaji Dar es Salaam. Mkuu wa
Upelelezi mkoa wa Rukwa SSP. Peter Ngussa amehamishiwa Makao makuu ya
Upelelezi Dar es salaam, nafasi yake inachukuliwa na SSP Alan Bukumbi
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Polisi
wilaya ya kati( OCD) Mrakibu wa Polisi (SP) Salum Ndalama anaenda kuwa
kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora na aliyekuwa mkuu wa Polisi wa
wilaya ya Tunduru (OCD) SP. Amadeus Tesha anakwenda kuwa Mkuu wa
upelelezi kikosi cha Polisi reli.
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
0 comments:
Post a Comment