Monday, November 18, 2013


pinda-kanisa-3 
Na Mwandishi Wetu
MAASKOFU wa makanisa mbalimbali nchini wametoa baraka zao za Tamasha la Krismas linalotarajia kufanyika Desemba 25 mwaka huu, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na baadaye kufanyika katika mikoa minne hapa nchini.
Viongozi hao wa makanisa nchini Tanzania kwa nyakati tofauti wameahidi kuliombea Tamasha la Krismas ili liwe la mafanikio yaliyotarajiwa kwa utukufu wa Mungu.
Wanasema  tamasha hilo ni muhimu hasa katika nyakati hizi za uasi mwingi ambapo dunia imekengeuka na kutenda matendo yanayomchukiza Mungu, kama vile vitendo vya ugaidi, uuzwaji wa madawa ya kulevya na mauaji ya watu wasio na hatia, hivyo tamasha hilo ili kurejesha utukufu wa Mungu mioyoni mwa watenda mabaya.
Tamasha la Krismasi ni muendelezo wa Tamasha la Pasaka lililoasisiwa tangu mwaka 2000 kwa lengo la kufikisha neno la Mungu kwa wananchi kwa njia muziki wa sifa na kuabudu.
Hatua ya kuandaliwa kwa Tamasha la Krismasi ni baada ya kuwepo kwa matokeo mazuri ya kupungua kwa matukio mbalimbali ya uhalifu na ukiukwaji wa kanuni hapa nchini, hiyo ni kufuatia Tamasha la Pasaka ambalo mwaka huu lilikwenda na kauli mbiu ya utii wa sheria pasipo shuruti.
Utofauti wa Tamasha la Krismasi na Tamasha la Pasaka ni kwamba tamasha hili waimbaji wote wataimba moja kwa moja ‘live’ lakini maudhui yatabaki kuwa yale yale kama ya tamasha la Pasaka kumwabudu na kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji.
Makamu Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk. Magnus Mhiche anasema Mungu amempa mzigo mzito Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama ambao anatakiwa awagawie waumini mbalimbali.
Sambamba na hilo Askofu Mhiche anampongeza Msama kwa hatua hiyo ya kuandaa matamasha ya kumtukuza na kumsifu Mungu.
Anasema tamasha hilo si la dhehebu moja bali  ni la Watanzania wote hivyo ni vema kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuweza kuomba kwa pamoja kupitia nyimbo.
Pia Askofu Mkuu wa Kanisa la Oasis of Healing, Prosper Ntepa, pamoja na kuliombea tamasha hilo aliwapongeza waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotions kwa kazi nzuri wanayoifanya katika uandaaji wa matamasha makubwa ya kumuabudu Mungu hapa nchini.
“Msama Promotions wanajitahidi katika uandaaji wa matamasha ya kumtukuza Mungu, tunazidi kumuombea afanikishe tamasha la krismas  ambalo linatarajia kufanyika kwenye mikoa mitano hapa nchini,” alisema Askofu Ntepa.
Askofu Ntepa pamoja na kutoa pongezi kwa Msama alitoa wito kwa waimbaji kutunga na kuimba nyimbo zenyemaudhui ya ujumbe mzito wenye tafsri halisi ya krismass,na mlengo wa kumtukuza na kumuabudu Mungu kwa njia ya sifa.
Askofu Ntepa anasema ili kufanikisha hilo waimbaji wanatakiwa kujitambua kwa jamii kwamba wanatakiwa kuwa mfano ambao utasaidia kufikisha neno la Mungu ambalo baadhi ya waimbaji  wanashindwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo tamaa ya pesa.
Aidha Askofu Ntepa anasema ili Msama kufanikisha hilo inatakiwa kuchagua waimbaji ambao wana dhamira ya kweli ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa waumini wengi zaidi.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Living Water Centre, Onesmo Ndegi alitumia fursa hiyo kumpongeza Msama kwa kufanikisha tamasha hilo ambalo ni mfano wa kuigwa kwa sababu linafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa maelfu ya Watanzania.
Askofu Ndegi alisema yeye pamoja na viongozi wenzake wa dini pamoja na waumini wake wanaungana na kumuombea Msama kwa sababu ni wajibu  kama ilivyo agizwa kwenye Biblia,  kwani tamasha hilo ni ibada tosha kwa waliookoka  ingawa jamii inapata burudani na kumsifu Mungu kupitia nyimbo.
“Mimi na kanisa langu nawaunga mkono Msama Promotions zaidi na nazidi kuwaombea kufanikisha Tamasha la Krismasi kwa sababu wengi watashiriki  ibada ipasavyo,” alisema Askofu Ndegi.
Mwangalizi  Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima anasema jambo lolote la kumuimbia na kumuabudu Mungu kupitia nyimbo ni jema.
Gwajima anawashambulia wale wote watakaotumia tamasha hilo kama sehemu uiba fedha kwani anaamini fedha zitakazopatikana kwenye tamasha hilo litasaidia jamii mbalimbali ya Watanzania kama ilivyoagizwa na mwandaaji ambaye ni Msama.
 “Tamasha la Krismasi ni sehemu ya mahubiri kwani kila anayehubiri anatakiwa kuyatekeleza yale anayoyahubiri  na si vinginevyo,” anasema Gwajima na kuongeza;
“Namuombea Msama na kampuni zake kufanikisha matamasha yake ambayo ni sehemu stahili katika kumtukuza na kumuabudu Mungu,”.
Mchungaji Christopher Mlaponi wa (TAG) Kinondoni Revival aliipongeza Msama Promotions kwa sababu wao ndiyo waandaaji wakuu wa Matamasha ya Kimataifa ya muziki wa injili kwa hatua waliyofikia.
Mchungaji Christopher, anasema kampuni hiyo inastahili pongezi kwa kuanzisha Tamasha la Krismasi kwa kuwa lina manufaa makubwa katika jamii hasa katika siku hizo za sikukuu ya Krismasi.
Anasema jambo la busara kwa kampuni hii kuanzisha matamasha ya muziki wa injili kwa siku kama hizi ambapo aliwataka waumini kuitumia siku hiyo kusheherekea Krismasi kwa kumtukuza Mungu kwa kushiriki katika tamasha hilo na si kufanya vitendo viovu.
“Hii siku siyo ya kula na kunywa, au kufanya anasa hapana, isipokuwa watu wanatakiwa kwenda makanisani asubuhi kama inavyohitajika wakirudi wajumuike katika Tamasha la Krismasi kwani wanapata neno la Mungu kupitia nyimbo za injili” anasema .
Anasema hiyo siku hutokea mara moja kwa mwaka hivyo Wakristo wanatakiwa wamtukuze na kumuimbia Yesu kwenye tamasha hilo.
Naye Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama anasema tamasha hilo ni muendelezo wa Tamasha la Pasaka, hivyo wadau wajiandae kupata ibada stahiki kwa waumini mbalimbali watakaofika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam  na wengine wa mikoa minne hapa nchini ambayo ni Morogoro, Dodoma, Tanga na Arusha.
“Tamasha la mwaka huu litashirikisha waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje, lengo likiwa ni ibada ambayo itawafikia waumini wote,” anasema Msama.
Msama anawataja waimbaji waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Eiphreim Sekereti huku waimbaji wengine wanaendelea na mazungumzo kwa ajili ya kuthibitisha kushiriki.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video