Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wanafunzi wa
shule ya sekondari ya kata ya Mgomba pamoja na walimu wao,Katibu Mkuu
alitembelea shuleni hapo kuona utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya
maabara .
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaidiana na fundi katika
kukamilisha hatua za mwisho za upigaji lipu wa wa jengo la maabara la
shule ya Sekondari ya kata ya Mgomba iliyopo wilayani Tunduru.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa kwenye
picha ya pamoja na wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari
ya Mgomba wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia shughuli za ubanguaji
korosho katika kiwanda cha kubangua korosho wilayani Tunduru.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akizungumza
na wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Tunduru ambao
walimweleza Katibu wa NEC kuwa wanalipwa kwa wiki na inategemea na idadi
ya kilo ulizobangua.
Katibu
Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuoka kwa meneja wa
kiwanda hicho Ndugu Shinoy jinsi kodi za vyama vya ushirika zinavyokuwa
mzigo kwao na kushauri bora zilipwe kwa mkulima moja kwa moja.
Pichani ni wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho wakiwa kazini
katika Kiwanda cha kubangua korosho cha Tunduru mkoani Ruvuma .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na mjumbe wa NEC wa
wilaya ya Tunduru Mzee Kalolo,tayari kwa ufunguzi wa ofisi ya CCM kata
ya Jakika jimbo la Tunduru Kaskazini.
Ofisi ya Kata ya Jakika jimbo la Tunduru Kaskazini ambayo imefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya
Jakika wakati wa ufunguzi wa ofisi ya kata ya Jakika iliyopo jimbo la
Tunduru Kaskazini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza wananchi wa kata ya Jakika kwenda kuwasha tanuri la kuchomea matofali.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuwasha moto katika
matanuri ya kuchomea matofali katika kata ya Jakika jimbo la Tunduru
Kaskazini.
Wananchi
wakimpa mikono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kama ishara
ya kumkaribisha katika kijiji cha Matemanga wilaya ya Tunduru.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye wakiongoza wananch wa Matemanga kwenda kusaidia
shughuli za ujenzi wa nyumba mbili za madaktari ambazo zinajengwa na
Taasisi ya Rais Mstaafu Ndugu Benjamin Mkapa.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia
wakazi wa kijiji cha Matemanga wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu
Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za pongezi kwa taasisi ya
Rais Mstaafu Ndugu Benjamin William Mkapa kwa ujenzi wa nyumba mbili za
kuishi madaktari katika kituo cha Afya cha Matemanga wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa mkono wa shukrani kwa fundi
Denis Ngaiza baada ya kutoa ushirikiano wa kutosha katika ujenzi wa
nyumba za Madaktari wa kituo cha afya cha Matemanga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha
Milonde kata ya Matemanga katika kituo cha Kihuma wilaya ya Tunduru
mkoani Ruvuma.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro, Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma Thabit Mwambungu na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo
Mwisho wakipitia kwa makini mambo mbali mbali katika nyaraka muhimu za
taasisi ya huduma ya ya kiroho na kibinadamu ya Kihuma iliyopo wilaya ya
Tunduru mkoani Ruvuma
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga kinanda wakati wanakwaya wa kikundi cha Kihuma wakitumbuiza .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la
ofisi ya kata ya Mlingoti Mashariki wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Sehemu ya umati uliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM katika viwanja
vya Baraza la Eid wilayani Tunduru ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndgu
Abdulrahman Kinana alihutubia.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia umati wa wakazi wa
wilaya ya Tunduru waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Baraza la
Eid, Nape aliwaambia wana Tunduru ni jukumu letu kulinda amani ya nchi
na kutaka watu wasikubali kupotoshwa katika mchakato wa kupata Katiba
Mpya.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho akihutubia wakazi wa Tunduru
kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuja
kuhutubia.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi
katika viwanja vya Baraza la Eid wilayani Tunduru ambapo aliwaeleza
wananchi hao kuwa CCM ni chama cha kutetea haki za wakulima na
wafanyakazi na kuwambia wananchi hao kuwa kila kilichoahidiwa
kitatimizwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Thabit Mwambingu akihutubia wananchi wa Tunduru
namna Serikali inavyofungua mkoa wa Ruvuma kwa kuongeza na kujenga
barabara na kuongeza matumizi ya anga.
Mbunge
wa Tunduru Kaskazini Ndugu Ramo Matala akihutubia wakazi wa Tunduru na
kuwaambia taratibu za kuuza zao la korosho kwa pesa taslimu pia namna
anavyosaidia shule na wananchi wakawaida wakiwemo walemavu ambao
alikabidhi baiskeli zao, vifaa vya michezo na kusaidia boda boda kupata
leseni.
0 comments:
Post a Comment