Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na
Vita Kawawa Mbunge wa jimbo la Namtumbo Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma
mara baada ya kumpokea kwenye kata ya Mchomoro, Abdulrahman Kinana yuko
katika ziara ya kikazi ya mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Njombe ambapo
ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye
na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
wakikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzina
kusikiliza matatizo ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi
kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katika ziara hiyo ya Wilaya za
Tunduru na Namtumbo wananchi wamelalamikia kuhusu bei ya zao la Korosho
ikiwa ni pamoja na Tumbaku, lakini pia wakalalamikia suala zima la
Mbolea, ambapo Mbunge wa jimbo la Namtumbo Vita Kawawa ametuhumu baadhi
ya viongozi wa vyama vya ushirika na ofisa ushirika wa mkoa huo
kuwabambikizia madeni wakulima wa tumbaku kupitia ruzuku ya mbolea
ambapo makadirio ya mbolea inayohitajika kwa wakulima huongezwa
kinyemela na wananchi kuachiwa mzigo wa kulipa madeni ambayo hayawahusu
jambo ambalo linawatesa wakulima wa tumbaku na kuwaacha wakiwa hoi kiuchumi
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akipata
kifungua kinywa nyumbani kwa mwenyekiti wa shina ndugu Hussein Rwambo wa
pili kutoka kulia katika kata ya Mchomoro, kulia ni Vita Kawawa Mbunge
wa Jimbo la Namtumbo, Kushoto aliyekaa ni Dr. Asga Rose Migiro Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na aliyesimama mlangoni ni Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto ,
Vita Kawawa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo kulia na Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Ruvuma Oddo Mwisho wakichanganya Udongo wakati wakishiriki katika
ujenzi wa Wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambayo
inajengwa.
Kutoka kulia ni Vita Kawawa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi, Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Dr. Asha Rose Migiro
wakishiriki katika ujenzi wa msingi wa wodi ya wazazi katika hospitali
ya wilaya ya Namtumbo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kushiriki ujenzi wa msingi wa wodi ya wazazi katika
hospitali ya wilaya ya Namtumbo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Vita Kawawa Mbunge
wa jimbo la Namtumbo wakati alipokuwa akikagua majengo ya hospitali
hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mkuu wa mkoa wa
Ruvuma Ndugu Said Mwambungu mara baada ya kukagua mtambo wa kuteketeza
takataka na kuchemsha maji katika hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata taarifa ya mtambo wa kufua umeme katika kituo cha kufua umeme cha Namtumbo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na watumishi wa kituo cha kufua umeme mjini Namtumbo.
Dr.
Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa
mjini Namtumbo leo.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi
katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa taifa mjini Namtumbo leo.
Wazee
wa kimlia wakimvisha mgolole Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana kama ishara ya heshima kwake kutokana na utendaji kazi uliotukuka
katika chama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa leo.
Mbunge
wa Jimbo la Namtumbo Mh. Vita Kawawa akiwahutubia wananchi kwenye
mkutano wa hadhara mjini Namtumbo, mkutano huo umefanyika kwenye uwanja
wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment