TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana
amesikitishwa na taarifa ya kifo Cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Dr Sengondo Mvungi kilichotokea Jana katika Hospitali ya Millpark
nchini Afrika ya Kusini.
Kwa
niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu anawapa pole wanafamilia,
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba na Uongozi wa
Chama Cha NCCR-Mageuzi. Hakika Taifa limepoteza Mtaalamu wa Sheria,
Kiongozi Mzalendo na hodari katika kipindi ambacho mawazo yake yanahitajika kwa kiasi kikubwa kuliendeleza Taifa hili.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
Imetolewa na:
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
0 comments:
Post a Comment