Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone akizungumza kwenye mkutano wa wadau
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach hoteli mjini
Singida.
Mjumbe
wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Lyidia Choma (kulia)
akitoa taarifa yake kwenye siku ya wadau wa Mfuko huo na ule wa Afya ya
Jamii (CHF).Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala
Beach Hotel mjini Singida. Kushoto (aliyeshika mike) ni Meneja wa NHIF
mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
Mkurugenzi
wa takwimu na uhai wa mfuko wa NHIF makao makuu, Michael Mhando akitoa
nasaha zake kwenye mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
Katala Beach Hotel mjini Singida. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa
Singida,Dk.Parseko Kone, Wa kwanza kulia ni kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa
Singida,Dk.Mussa Kamala, Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi na
katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, (wa pili kulia) akifuatilia kwa
makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano wa siku ya wadau wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii. Wa kwanza
kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Lyidia
Choma.Wa tatu kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan
na,Mkuu wa Wilaya ya Singida,Queen Mlozi na kaimu Mganga Mkuu mkoa wa
Singida,Dk.Mussa Kimala.
Na Nathaniel Limu
Zaidi ya asilimia 73 ya kaya
za mkoa wa Singida, hazijajiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF), hali
inayochangia wanafamilia watibiwe bila utaratibu maalum.
Hayo yamesemwa na mkuu wa moa
wa Singida, Dk. Parseko Kone, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa
mkutano wa siku ya wadau wa Mfuko wa Taifa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya
ya Jamii (NHIF) wa mkoa wa SIngida.
Akifafanua, amesema kati ya
kaya 259,251 za mkoa wa Singida, ni kaya 45,575 tu, ndizo zilizojiunga
na mfuko wa afya ya jamii kati ya mwaka 1998 na Septemba 30 mwaka huu.
Hii ni sawa na asilimia 17.6 tu.
“Hata hivyo,wilaya ya Iramba
imekuwa ikifanya vizuri katika uandikishaji wa wananchi, kwani takwimu
zinaonyesha hadi Septemba 30 mwaka huu, wamekwisha andikisha asilimia
50.3 ya kaya zilizolengwa. Hali hii inaonyesha kuwa viongozi bado
hatujatimiza wajibu wetu wa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huu”,
amesema Dk.Kone.
Aidha, mkuu huyo wa mkoa,
amesema pia inawezekana watoa huduma wamekuwa ni chanzo cha kuwakatisha
tama wananchi waliojiunga na hivyo, kuwafanya wananchi wengine wasite
kujiunga na Mfuko huu.
“Kwa kuwa wadau wote
tumekutana hapa leo, ni nafasi yetu kuangalia nini sababu ya kuzorota
kwa utaratibu huu ambao katika baadhi ya halmashauri hapa nchini,
umeimarika zaidi”,amesema Dk.Kone.
Awali mjumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Lyidia Choma,
alisema Mfuko huo umeidhinisha shilingi bilioni 10, ili zitolewe kwa
watoa huduma kuwawezesha kupata vifaa tiba na kukarabati maeneo yao ya
kutolea huduma.
“Utaratibu huu ni mikopo ya
bei nafuu ambayo hairejeshwi kwa fedha taslimu, isipokuwa kwa kukatwa
katika madai ambayo mtoa huduma anawasilisha kwa Mfuko”,amefafanua.
Alifafanua kuwa kwa mkopo wa
vifaa tiba, mkopo hurudishwa kwa makato ya asilimia 10 ambayo hulipwa
ndani ya miezi 24 na mikopo ya ukarabati wa maeneo ya kutolea huduma, ni
miezi 36.
Kauli mbiu ya mwaka huu, ni Afya Bora kwa wote sasa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
0 comments:
Post a Comment