Na.Ngonise Kahise
Mwakilishi wa kampuni ya Delina Group (DGE) kushoto,Bw. Emmanuel Mzava,akionyesha waandishi wa habari vifaa
vya michezo vilivyotolewa na Bw. Davis Mosha. Kulia ni Mkurugenzi wa
Swahili Media International, MMK Media Group Bw. Alex Kassuwi (kulia).
Kampuni
ya Delina Group (DGE) inayomilikiwa na Bw. Davis Mosha imekabidhi vifaa
vya michezo vyenye thamani ya mamilioni ya pesa pamoja na vikombe kwa
ajili ya kumtafuta Bingwa wa Uhuru Cup kwa timu za mpira ambazo
zinaundwa na watanzania ambao wanaishi nchini Marekani na ni mashabiki
wa Simba na Yanga. Tarehe za mechi hizo zitatajwa hivi karibuni
tukishirikianana ubalozi wa Tanzania.
Mwakilishi
wa kampuni ya Delina Group (DGE) kushoto,Bw. Emmanuel Mzava,akimkabizi
vifaa vya michezo,mwakilishi wa mashabiki wa Simba na Yanga wanaoishi
Marekani Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media Group Bw.
Alex Kassuwi (kulia).
Aidha
Emmanuel ameongeza kuwa,lengo la Kampuni ya Delina Group (DGE)
kudhamini timu hizo zinazoundwa na mashabiki wa Simba na Yanga zilizopo
ugenini,ni kuweka hamasa ya ushindani ndani na nje ya nchi,na kuongeza
kuwa zoezi hilo ni endelevu.
kutoka kushoto ni Emmanuel Mzava wa Delina Group (DGE) na kulia anayezungumza ni
Alex Kassuwi Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media Group wamiliki wa Swahili Radio Online, Swahili TV online, Swahilitv blog, na DMK411 blog
Alex Kassuwi Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media Group wamiliki wa Swahili Radio Online, Swahili TV online, Swahilitv blog, na DMK411 blog
0 comments:
Post a Comment