Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
BENCHI
la ufundi la wakata miwa wa Kaitaba, wana Nkulukumbi Kagera Sugar
limesema kikosi chake kwa kiasi kikubwa kinakidhi mahitaji yao, ingawa
wana mpango wa kuongeza nyota wachache hasa sehemu ya ulinzi na kiungo.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Murage Kabange amesema wachezaji watakaoongezwa ni wa hapa hapa Tanzania.
“Ukiangalia
kikosi chetu, tumesajili wachezaji 24 tu, na kati yao wawili ni kutoka
Uganda, hatuna sababu ya kuongeza wachezaji kutoka nje, tunataka
wachezaji wa Tanzania”. Alisema Kabange.
Kabange
ameongeza kuwa kilichowaathiri mzunguko wa kwanza ni wachezaji
kutoelewana kwani kulitokea mabadiliko kwani kuna wachezaji wao
waliondoka na walisajiliwa wapya, lakini mzunguko wa pili watarudisha
makali yao.
“Mzunguko
wa pili tutarudi na kasi kubwa kama msimu uliopita, kikosi ni kilekile,
malengo yetu na kushika nafasi za juu. Tumeshagundua mapungufu yetu,
tulichelewa kuanza matayarisho, wachezaji wa zamani walibaki 14,
tuliongeza wapya karibu 10, na tulichelewa kuanza kuunganisha kikosi”.
Alisema Kabange.
Kocha
huyo msaidizi aliwataka mashabiki wa soka mkoani Kagera kuwapa sapoti
kubwa kwani timu yao inajipanga kuwapa raha kubwa mzunguko wa pili wa
ligi kuu Soka Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment