KLABU
ya Manchester United imepata pigo kubwa baada ya nyota wa Barcelona
iliyekuwa inamtaka, Andres Iniesta kukubali kusaini Mkataba mpya na
klabu yake hiyo ya Hispania.
Mkurugenzi
wa Michezo wa Barca, Andoni Zubizarreta amesema kiungo huyo yuko karibu
kusaini Mkataba mpya na vinara hao wa La Liga.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 29 ilielezwa hafurahii maisha Nou Camp
kutokana na kutofautiana na mabosi wa timu hiyo, hivyo kumpa matumaini
kocha David Moyes, ambaye amekuwa akimmezea mate na kutaka kumsajili
Januari.
Pamoja na hayo, kipa wa zamani wa Barca, Zubizarreta amepuuza madai kwamba Iniesta ataihama klabu hiyo.
Anabaki? Andres Iniesta ilielezwa hafurahii maisha Barcelona, lakini sasa imeelezwa atasaini Mkataba mpya
Pigo: Kocha wa Manchester United, David Moyes (juu) ilielezwa anataka kumsajili Iniesta Januari
0 comments:
Post a Comment