Mratibu
Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima (kushoto) akizungumza
kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya
Pera Bw. Rashid Kiwamba (kulia) kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo
ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake
wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za
kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
.Zaidi ya wanawake 220 wafikiwa na mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani
Na Damas Makangale, Chalinze Moblog
SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO)
limeendesha mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika
juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. Moblog
inaripoti.
Mradi huo wa Shirika la Kazi
Duniani (ILO) unalenga wanawake wote ambao wapo pembezoni wa barabara na
mipakani kwa sababu wapo katika hali ya hatarishi.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari Mkoa Pwani Wilayani Chalinze, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi
kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Getrude Sima amesema ndani ya siku
sita mradi wa mapambano ya Ukimwi chini ya ILO umewafikia wanawake 120
katika kata za Pera, Chamakweza, Mpingo, Bwilingu, Msolwa na Mdaula.
Mshauri
wa Biashara wa shirika lisilokuwa la Kiserikali (NGO) TAPBDS Bi.
Theresia Kato akifundisha wakinamama wa Chalinze (hawapo pichani) jinsi
ya kuandika na kuandaa mchanganuo wa biashara katika mafunzo hayo ya
siku sita yaliyoandaliwa na Shirika la kazi Duniani (ILO).
Amesema
tangu mradi uanze kutekelezwa hapa nchini wakutoa mafunzo ya
ujasiriamali na kujikinga na Virusi vya Ukimwi wameweza kuwafikia
wanawake 220 nchi nzima katika maeneo ya pembezoni na mpakani kama vile
Tunduma, Kyela na Namanga.
“Unajua
wanawake wengi wanakuwa katika kundi hatarishi pale wanapokuwa katika
maeneo ya mpakani na pembezoni mwa barabara kwa mfano Chalinze kwa
sababu ya muingiliano wa watu hasa Madereva na Wafanyabiashara,” amesema
Sima.
Sima
ameongeza kuwa katika mradi huu wa mapambano ya Ukimwi malengo ni
kumuelimisha Mwanamke ili ajitambue na aweze kujikinga na maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi kwa kumfundisha stadi za maisha pamoja na
ujasiriamali.
Amesema
mradi unalenga wanawake wasiokuwa katik ajira rasmi ili kuongeza
muamuko miongoni mwa wakinamama mitaani na vijijini ili waweze
kukabiliana na vishawishi katika sehemu zao wanazoishi.
Bi. Theresia Kato akiwaelekeza washiriki namna ya kujaza fomu za kuombea mikopo kwa taasisi mbalimbali.
Kwa
upande Mshauri wa Biashara toka shirika lisilo kuwa la Kiserikali
TAPBDS, Theresia Kato amesema kuwa biashara ndogo ndogo ni muhimu katika
kumjengea mwanamke uwezo wa kujiamini na kujitegemea.
“lazima
wanawake waamuke ili waweze kuanzisha biashara zao na kuandika
mchanganuo wa biashara na kutafuta mitaji kupitia taasisi mbalimbali za
fedha hapa nchini,” amesema.
Mratibu
Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Bi. Getrude Sima akisisitiza jambo kwa
washiriki kuhusiana na mafunzo waliyoyapata yakawe chachu ya kuleta
maendeleo.
Picha juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa Chalinze wakifuatilia mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.
Mgeni
rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba
akikabidhi vyeti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo.
Mwanamke wa Kimasai Paspen Kisota akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
Picha
juu na chini mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera
Bw. Rashid Kiwamba na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude
Sima wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu.
Fundi
Sanifu wa Maabara ya Afya Bw. Rwezahura Merehiory akichukua damu kwa
ajili ya vipimo vya VVU kwa mmoja wa washiriki wa semina ya mafunzo ya
Ujasiriamali na Kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
iliyoratibiwa na shirika la Kazi duniani (ILO) wilaya ya Chalinze
mwishoni mwa wiki.
0 comments:
Post a Comment